Pata taarifa kuu
DRC-EBOLA-AFYA-WHO-CHANJO

Chanjo ya pili yaanza kuwasili nchini DRC

Mtalaam wa Ebola nchini DRC
Mtalaam wa Ebola nchini DRC REUTERS/James Akena

Wizara ya afya nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, inasema tayari shehena ya kwanza ya chanjo mpya ya Ebola imewasii nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Maafisa wa afya katika Mkoa wa Kivu Kaskazini wamesema kuwa dozi 11,000 ya chanjo ya pili ya Ebola iliyotengezwa na kampuni ya Johnson & Johnson iliwasili siku ya Ijumaa.

Dozi nyingine zaidi ya 40,000 inatarajiwa kuwasili Mashariki mwa nchi hiyo, kabla ya kuanza kutolewa katika eneo hilo ambalo maambukizi ya Ebola, yamesababisha watu zaidi ya 2,000 kupoteza maisha na wengine 3,000 kuambukizwa tangu mwezi Agosti mwaka 2018.

Tangu kuzuka kwa ugonjwa huo, maafisa wa afya wanasema kuwa watu zaidi ya 240, 000 walipata chanjo ya kwanza ya ugonjwa huu hatari.

Jean-Jacques Muyembe, anayeongoza kamati ya kupambana na Ebola,tayari ametangaza kuwa, chanjo hii mpya, itaanza kutolewa katikati ya mwezi huu.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.