Pata taarifa kuu
ALGERIA-MAANDAMANO-SIASA-UCHAGUZI

Maandamano makubwa kupinga uchaguzi yaendelea Algeria

Wagombea watano kuwania katika uchaguz wa urais Algeria, nchi ambayo inaendelea kukumbwa na maandamano makubwa ya kiraia, Novemba 2, 2019.
Wagombea watano kuwania katika uchaguz wa urais Algeria, nchi ambayo inaendelea kukumbwa na maandamano makubwa ya kiraia, Novemba 2, 2019. REUTERS/Ramzi Boudina

Wagombea 5 wakiwemo mawaziri wakuu 2 wa zamani, wanawania kuziba nafasi ya rais wa Algeria aliyeondolewa madarakani, Abdelaziz Bouteflika, imesema taarifa ya tume ya uchaguzi wakati huu kukishuhudiwa maandamano kupinga uchaguzi huo.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa tume ya uchaguzi nchini Algeria, jumla ya wagombea 23 waliwasilisha nyaraka za kuomba kuteuliwa kuwania kiti cha urais, lakini ni wagombea watano peke yake ndio majina yao yaliidhinishwa.

Mawaziri wakuu wa zamani, Ali Benflis na Abdelmadjid Tebboune, wanatarajiwa kuongoza katika uchaguzi ambao unapingwa vikali na maelfu ya wananchi ambao wameendelea kujitokeza barabarani.

Wanaharakati nchini humo wanashinikiza kufanyika kwa mabadiliko makubwa ya kisiasa kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu, wakisema washirika wakubwa wa Bouteflika bado wamesalia madarakani.

Wagombea hao sasa majina yao yamepelekwa kwa baraza la kitaifa kwa ajili ya kutathminiwa kabla ya kuthibitishwa rasmi kuwa wagombea.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.