Pata taarifa kuu
MALI-USALAMA

Mashambulizi Mali: Rais wa Mali wataka wananchi kuunga mkono vikosi vya usalma na ulinzi

Rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keïta akilihutubia taifa, Novemba 5, 2019.
Rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keïta akilihutubia taifa, Novemba 5, 2019. Capture d'écran

Baada ya mashambulio yaliyosababisha vifo vingi katika maeneo ya Boulikessi, Mondoro, na hivi karibuni katika eneo la Indelimane, rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keïta, kwa mara ya kwanza, amelihutubia taifa, huku akilaani waliohusika na mashambulizi hayo.

Matangazo ya kibiashara

"Mashambulio ya Indelimane, Boulikessi, Mondoro na mengine ambayo yalitangulia yanaonyesha hali ya wasiwasi inayoikabili Mali. Tuko vitani, "amesema Ibrahim Boubacar Keita.

Kundi la Islamic State (IS) lilidai kuhusika na shambulio dhidi ya kambi ya jeshi ya Indelimane.

Baada ya mashambulizi hayo kusababisha vifo vingi, rais wa Mali amelitaka jeshi kuwa na umoja: "katika mazingira ambayo ni mabaya ambapo utulivu na uwepo wa nchi yetu uko hatarini, jibu letu linapaswa kuwa la umoja wa kitaifa, umoja katika jeshi letu, "Boubacar Keita amesema akisisitiza.

Amebaini katika hotuba hiyo kwamba hivi karibuni alifanya mkutano na viongozi wote wa jeshi. Ujumbe wake uliwataka viongozi hao kubadilisha mkakati katika uwanja wa vita dhidi ya adui.

"Niliagiza hatua kadhaa kali, hasa kutumia mbinu nyingine mpya ambayo itawezesha jeshi letu kuwa na uwezo wa kukabiliana hadi kuangamiza adui popote alipo, " amesema.

Rais IBK amesema, vita dhidi ya ugaidi sio suala la Mali tu: "Vita hii sio vita tu dhidi ya Mali au Sahel, ni ya ulimwengu mzima. Katika uhali hii ya ukosefu wa usalama dunia, juhudi za pamoja na kuweka nguvu pamoja ni muhimu kwa kukabilina na hali hiyo, "ameongeza rais wa Mali.

Tutawakumbuka askari wa Mali waliouawa vitani, pia tutawakumbuka askari wa kigeni, hasa askari wa Ufaransa, waliouawa waiwa kazini nchini Mali, amebaini Rais wa Mali.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.