Pata taarifa kuu
SOMALIA_MAFURIKO-MAJANGA YA ASILI

Mafuriko Somalia: Misaada yaendelea kuwafikia walengwa

Somalia inaendelea kukabiliwa na mafuriko kutokana na mvua nyingi zinazonyesha.
Somalia inaendelea kukabiliwa na mafuriko kutokana na mvua nyingi zinazonyesha. Google Maps

Operesheni kubwa ya misaada inaendelea hivi sasa nchini Somalia kuwasaidia maelfu ya raia ambao wameathirika pakubwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Maeneo yanayotajwa kuathirika pakubwa ni pamoja na kwenye mji wa Beled weyne unaopakana na nchi ya Ethiopia, ambapo picha za video zimewaonesha wananchi wakiwa wamenasa juu ya paa za nyumba zao huku karibu mji mzima ukifunikwa na maji.

Nchi za Tanzania, Kenya, Sudan na Ethiopia, ni miongoni mwa mataifa mengi ya ukanda wa Afrika Mashariki na pembe ya Afrika ambazo zimeshuhudia mafuriko.

Mvua kubwa isiyo ya kawaida na mafuriko yamezidi kukumba Somalia, Sudan Kusini na Kenya mwaka huu. Watabiri wa hali ya hewa wanatarajia mvua hiyo kubwa kuendelea kunyesha hadi Desemba.

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani, WFP linashirikiana kwa karibu na wizara ya inayohusika na masuala ya kibinadamu na majanga nchini Somalia na pia mashirika mengine ya serikali.

Tayari WFP imetuma helikopta kusaidia shughuli za kibinadamu kati ya Beletweyne na sehemu zilizo karibu zilizoathiriwa vibaya na mafuriko kutoka mto Shabelle.

WFP ina mpango wa kusaidia familia 4,000 kutoka vijiji saba kwenye wilaya ya Beletweyne.

Wakati wa ziara yake huko Belet Weyne, Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed 'Farmaajo' ameelezea wasiwasi wake juu ya kiwango cha madhara yaliyosababishwa na mafuriko na kile kinachohitajika kukwamua maeneo husika.Amesema kwamba wanafahamu mafuriko ya mwaka jana yalivunja rekodi lakini pengine haya ya mwaka huu yatakuwa na madhara makubwa zaidi.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.