Pata taarifa kuu
DRC-BENI-SIASA-USALAMA-ADF

DRC: Watu wanne wapoteza maisha wilayani Beni baada ya kushambuliwa na waasi

Waasi wa ADF Nalu
Waasi wa ADF Nalu Reuters

Raia wanne wamepoteza maisha wilayani Beni, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, baada ya kushambuliwa na waasi waliojihami kwa silaha.

Matangazo ya kibiashara

Haya yanajiri, baada ya jeshi kusema kuwa, limewauawa waasi 25 wa ADF Nalu katika eneo hilo la Beni.

Shambulizi hilo lilitokea katika eneo la Eringeti, Kilomita 60 kutoka Beni, sehemu ambayo imeendelea kuwa ngome ya waasi wa ADF, kwa mujibu wa msemaji wa jeshi Mak Hazukai.

Ndani ya wiki moja, maafisa wa usalama wanasema, waasi 25 wameuwa huku wanajeshi sita nao wakipoteza maisha.

Tayari jeshi la DRC, limetangaza opersheni dhidi ya makund ya waasi katika eneo hilo kwa lengo la kurejesha hali ya usalama.

Tangu mwaka 2014 kundi la ADF limeendelea kushtumiwa kutekeleza mauaji na kusababisha maelfu ya watu kuyakimbia makwao.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.