Pata taarifa kuu
G5 SAHEL-UFARANSA-USALAMA

Nchi za G5 Sahel zataka kuungwa mkono kutokomeza makundi ya kigaidi

Marais Ibrahim Boubacar Keïta, Idriss Déby na Mahamadou Issoufou pamoja na Emmanuel Macron kwenye ikulu ya Élysée Novemba 12, 2019.
Marais Ibrahim Boubacar Keïta, Idriss Déby na Mahamadou Issoufou pamoja na Emmanuel Macron kwenye ikulu ya Élysée Novemba 12, 2019. © JOHANNA GERON / POOL / AFP

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amethibitisha kuwa nchi yake itafanya kila jitihada kuhakikisha operesheni za kijeshi zinazolenga kuyatimua makundi ya wanajihadi kwenye ukanda wa Sahel zinafanikiwa.

Matangazo ya kibiashara

Kauli hii ya Macron imetolewa hapo jana wakati akikutana na viongozi wa mataifa 5 yanayojumuika katika ukanda huo wa Sahel, ambao wanashiriki mkutano wa amani ulioanza hapo jana jijini Paris.

Viongozi wa Mali, Niger na Chad wametetea hatua yao katika mapambano dhidi ya ugaidi wakati wa mazungumzo ya hadhara. Mbali na hatua za kijeshi zinazohitajika kukabiliana na makundi yenye silaha, marais wa nchi hizi tatu wamesisitiza umuhimu wa maendeleo kwa sababu, umasikini unachiochea ugaidi, wamesema.

Hata hivyo Rais wa Nigera Mahamadou Issoufou amesem abado uwezo unakosekana katika kupambana vilivyo na makundi hayo.

"Mara nyingi tunasikia wakosoaji wakisema:" G5 Sahel haina mkakati, wakuu wa nchi wa G5 Sahel hawana mkakati. " Tuna mkakati lakini tunakosa uwezo ambao utatuwezesha kutekeleza mpango huo, "amesema rais wa Niger.

Rais Macron amesema anaendelea kuyahimiza mataifa mengine ya ulaya kutekeleza ahadi zao kuhusu michango yao ya hali na mali katika kufanikisha operesheni hizo,

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.