Pata taarifa kuu
SUDANI-ICC-BASHIR-SIASA-HAKI

Sudani: Rais wa zamani Omar al-Bashir hatafikishwa ICC

Rais wa zamani wa Sudan Omar al-Bashir katika mahakama ya KhartoumAgosti 31, 2019.
Rais wa zamani wa Sudan Omar al-Bashir katika mahakama ya KhartoumAgosti 31, 2019. © REUTERS/Mohamed Nureldin Abdallah

Kwa wiki kadhaa kumekuwa na uvumi kuhusu uwezekano wa rais wa zamani wa Sudani Omar Hassan al-Bashiri kufikishwa kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai, mjini Hague, kujibu tuhuma dhidi yake.

Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo, Rais wa Baraza Kuu Tawala nchini Sudani, Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, amebaini kwamba Omar Hassan al-Bashir hatofikishwa kwenye mahakama hiyo.

Kauli hii ya Jenerali Abdel Fattah al-Burhan imewaacha vinywa wazi wanaharakati wa haki za binadamu nchini humo, hasa wale kutoka Jimbo la Darfur.

Omar al-Bashir anasakwa na waranti wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai, ICC, kwa uhalifu wa kivita, uhalifu dhidi ya binadamu na mauaji ya kimbari katika Jimbo la Darfur.

Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai, ICC, haina shinikizo lolote kwa Sudani, alikumbusha balozi wa Sudani kwenye Umoja wa Mataifa, huku akibaini kwamba Khartoum haikutia saini kwenye mkataba wa Roma unaounda mahakama hiyo.

Alipozuru Darfur wiki tatu zilizopita, Waziri Mkuu wa Sudani Abdalla Hamdok aliwapa matumaini wakaazi wa jimbo hilo. Mbele ya wakimbizi waliomba wahalifu wote wa Darfur wapelekwe ICC, Abdalla Hamdok alijibu: "Sote tutafanya kazi kwa pamoja ili kutosheleza maombi yenu na kuhakikisha kurudi kwa maisha ya kawaida. "

Kauli hii ilikaribishwa na mashirika ya kiraia nchini humo.

Omar al-Bashir hivi sasa anakabiliwa na kashfa ya ufisadi nchini humo. Uamuzi unatarajiwa kutolewa mwezi ujao. Omar al-bashir pia anakabiliwa na tuhuma za kuhusika kwake katika jaribio la mapinduzi lililomfikisha madarakani miaka 30 iliyopita, kosa ambalo hukumu yake ni kunyongwa au kifungo cha maisha.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.