Pata taarifa kuu
GUINEA BISSAU-UCHAGUZI-SIASA-USALAMA

Domingos S. Pereira na Umaro S. kukabana koo katika duru ya pili ya uchaguzi Guinea-Bissau

Domingos Simões Pereira alishinda kwa 40% ya kura kulingana na matokeo ya awali.
Domingos Simões Pereira alishinda kwa 40% ya kura kulingana na matokeo ya awali. © PAULO CUNHA/LUSA

Duru ya pili ya uchaguzi wa urais itawakutanisha wagombea wawili maarufu nchini Guinea Bissau, baada ya mshindi kukosekana katika duru ya kwanza ya uchaguzi huo. Wagombea wote wawili hawakutimiza idadi ya kura inayohitajika, kushinda katika duru ya kwanza.

Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo tume ya uchaguzi nchini Guinea Bissau imetangaza Jumatano asubuhi matokeo ya awali ya uchaguzi wa urais uliyfanyika Jumapili Novemba 24.

Mgombea wa chma cha PAIGC anayeongoza katika uchaguzi huo, Domingos Simões Pereira, atamenyana na Umaro Sissoco Embalo.

Domingos Simões Pereira (DSP), amepata asilimia 40.13 ya kura dhidi ya 27.65% alizopata Umaro Sissoco Embalo, anayepeperusha bendera ya chama cha MADEM, chama cha kwanza cha upinzani bungeni.

Saa chache baada ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi, Pereira alitoa wito kwa mgombea wengine kujiunga katika mchakato wa ucahguzi, hasa kuwaunga mkono wagombea katika duru ya pili ya uchaguzi.

"Tunatolea wito wagombea wengine kujiunga nasi. Tunahitaji kila mmoja kushiriki katika ujenzi wa taifa letu, Guinea-Bissau, " amesema Pereira.

Duru hii ya pili inawakutanisha mawaziri wawili wakuu wa zamani, uchaguzi ambao umepangwa kufanyika Desemba 29, 2019.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.