Pata taarifa kuu
DRC-MAUAJI-USALAMA

Shambulio la ADF laua watu kadhaa Mashariki mwa DRC

Askari wa Umoja wa Mataifa nchini DRC, MONUSCO, huko Beni, DRC, Novemba 26, 2019.
Askari wa Umoja wa Mataifa nchini DRC, MONUSCO, huko Beni, DRC, Novemba 26, 2019. ALBERT KAMBALE / AFP

Wapiganaji wa kundi la waasi wa Uganda, ADF, wamefanya shambulio jipya katika wilaya ya Beni Kaskazini Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Watu 22 wameuawa katika tarafa za Ndombi na Kamango.

Matangazo ya kibiashara

Mauaji hayo yanafikisha idadi ya watu 33 kuuwawa na waasi waliojihami chini ya saa 24.

Hata hivyo mamlaka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo zinasema kuwa watu 11 wameuawa usiku wa kuamkia leo katika eneo la Beni Mashariki mwa nchi hiyo.

Wanawake 13 ni miongoni mwa watu 22 waliouawa na waasi wa ADF usiku wa Jumamosi.

Zaidi ya raia 180 wameuwawa tangu mwezi Oktoba mwaka huu wakati jeshi lilipotangaza operesheni dhidi ya makundi ya wanamgambo wenye silaha wanaotuhumiwa kutekeleza mashambulizi dhidi ya raia.

Mauwaji haya yanaendelea wakati jeshi la serikali linaendesha operesheni  dhidi ya ADF, lakini wadadisi wa masuala ya usalama wanasema kuna uzembe katika uongozi wa jeshi hasa katika operesheni zinazotajwa na jeshi la Serikali kuwa ndio za mwisho kufanyika katika eneo hili, ili kuwaangamiza waasi wa ADF.

Mashambulio ya hivi karibuni yamezua hasira na maandamano makali miongoni mwa wakaazi amabo wanalaumu vikosi vya kulinda usalama vya umoja wa mataifa kwa kutowahakikishia usalama.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.