Pata taarifa kuu
DRC-TANGANYIKA-ELIMU

Fedha za kuwalipa mshahara Walimu zaibiwa katika jimbo la Tanganyika

Waalimu wa Kabalo walalamika wizi wa mishahara yao na wanadai walipwe. (picha ya kumbukumbu)
Waalimu wa Kabalo walalamika wizi wa mishahara yao na wanadai walipwe. (picha ya kumbukumbu) RFI/Sonia Rolley

Majambazi katika mtaa wa Kabalo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamepora karibu Dola Laki Moja, fedha ambazo zimeelezwa kuwa ni mshahara wa mwezi wa Desemba wa Walimu katika jimbo la Tanganyika.

Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa chama cha kutetea Walimu katika mkoa huo amesema kuwa tayari uchunguzi umeanzishwa ili kubaini waliotekeleza wizi huo.

Kakudji wa Ngoy, mhasibu wa Shule katika mtaa wa Kabalo pamoja na ujumbe wake, walikuwa wanarejea katika kijiji cha Kongolo ambacho alikuwa amepokea hizo fedha kutoka Benki, wakati waliposhambuliwa.

"Tulishambuliwa na watu waliokuwa na silaha, walifwatua risasi hewani na tukawa na wasiwasi ikabidi tukimbilie msituni na hapo ndipo walipochukua kila kitu," alisema Ngoy.

Hata hivyo, walimu katika mtaa huo wanasema kuwa hawaamini kuwa pesa hizo zimeibiwa na wanaendelea kusubiri mshahara wao.

"Hii sio mara ya kwanza kwa kisa kama hiki kutokea, kama tulivyoona mwaka jana,: alisema Fidele Mwalimwenze mmoja wa Walimu.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.