Pata taarifa kuu
SUDAN

SUDAN: Wanaharakati wapongeza hukumu ya mahakama

Waandamanaji wa nchini Sudan walipokuwa kwenye barabara za Khartoum, August 17, 2019.
Waandamanaji wa nchini Sudan walipokuwa kwenye barabara za Khartoum, August 17, 2019. AFP/Ahmed Mustafa

Wanasheria, wanaharakati na wananchi wa kawaida nchini Sudan, wameipongeza mahakama ya nchi hiyo kwa kuonyesha uhuru wake baada ya kutoa adhabu ya kifo kwa maafisa ishirini-na-tisa wa idara ya upelelezi  waliohusika na mauaji ya mwandamanaji mapema mwaka huu. 

Matangazo ya kibiashara

Miongoni mwa waliopongeza uamuzi huo wa mahakama ni Fatuma Salma Abdel ambaye alishiriki kikamilifu maandamano ya kumuondoa madarakani Omar al-Bashir.

"Ni hatua muhimu kuonyesha kwamba sheria inatekelezwa bila upendeleo ambapo ni jambo la kuridhisha na kufurahisha kwamba kuanzia sasa watu wanaadhibiwa na wataadhibiwa siku zijazo bila kubaguliwa kisheria", alisema moja ya wanaharakati maarufu wa kike nchini Sudan.

 El Ghasim Hussein, ni wakili aliyemwakilisha mwanaharakati aliyeuwa na maafisa wa upelelezi yeye anasema "Kusema kweli, wimbi la mabadiliko ya kisheria limeibuka Sudan. Shukran kwa mapinduzi yaliyotokea hapa Sudan mwaka huu".

Wananchi wa Sudan pia wamekuwa na maoni tofauti kuhusiana na hukumu hii kama moja ya raia hao wanavyoeleza hapa.

"Mimi binafsi sikuamini kwamba idara ya mahakama ya Sudan itakuwa na mabadiliko kuwa kile sisi wanaharakati na wananchi wa kawaida tunashuhudia leo".

Adhabu ya kifo kwa waliotekeleza mauaji ya mwandamanaji, ndiyo sisi sote tumekuwa tukisubiri kuona ikiteketezwa na mahakama huru.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.