Pata taarifa kuu
LIBYA-URUSI-UTURUKI-USALAMA-SIASA

Mazungumzo kati ya mahasimu wawili Libya kufanyika Urusi

Marshal Khalifa Haftar (kushoto) na kiongozi wa serikali yenye makao yake makuu Tripoli, Fayez el-Sarraj.
Marshal Khalifa Haftar (kushoto) na kiongozi wa serikali yenye makao yake makuu Tripoli, Fayez el-Sarraj. © Fethi Belaid, Khalil Mazraawi/AFP

Waziri Mkuu wa Libya Fayez el-Sarraj na mbabe wa kivita Mashariki mwa nchi iyo, Marshal Khalifa Haftar wanatarajiwa nchini Urusi kwa mazungumzo.

Matangazo ya kibiashara

Mahasimu hao wawili katika mzozo wa Libya wanatarajiwa jijini Moscow ili kuhakikisha kuwa wako tayari kusitisha mapigano, hatua iliyofikiwa mwishoni mwa wiki hii iliyopita.

Fayez el-Sarraj, kiongozi wa serikali ya umoja wa kitaifa ya Tripoli, na Marshal Khalifa Haftar, mbabe wa kivita, Mashariki mwa Libya, wanatarajia kukutana katika mji mkuu wa Urusi kwa mazungumzo yanayasubiriwa kwa hamu na gamu.

Mamlaka nchini Urusi imethibitisha kwamba mkutano kati ya mahasimu hao wawili katika mgogoro wa Libya umetarajiwa kufanyika leo Jumatatu chini ya upatanishi wa Urusi, lakini pia na Uturuki.

Kwa kuandaa upatanishi huu, mawaziri wa ulinzi na mambo ya nje wa nchi hizo mbili walikutana Jumatatu hii asubuhi jijini Moscow.

Kwa mujibu wa msemaji wa wizara ya Mambo ya nje ya Urusi, Maria Zakharova, viongozi hao kutoka Libya walitarajiwa kukutana nao wakati wa mchana kwa lengo la kuhitimisha rasmi mcahakato wa kusitisha mapigano.

Moscow, haijafanya jitihada peke yake kwa kuwakutanisha mahasimu hao wawili katika mgogoro wa Libya. Urusi imeungana na rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, ambaye hivi karibuni aliingia katika mgogoro wa Libya kwa kutangaza kutuma vikosi vitakavyosaidia serikali ya Tripoli.

Kwa upande wake, Moscow inamuunga mkono Marshal Haftar, hata kama inaendeleza ushirikiano mzuri na serikali ya Tripoli. Ikiwa usitishwaji huu wa mapigano utathibitishwa rasmi ndani ya saa chache zijazo, bila shaka itakuwa mafanikio ya kidiplomasia kwa Moscow na Ankara.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.