Pata taarifa kuu
LIBYA-URUSI-UTURUKI-USALAMA-SIASA

Libya: Marshal Haftar aondoka Urusi bila kusaini makubaliano ya kusitisha mapigano

Marshal Khalifa Haftar, kiongozi wa kijeshi Mashariki mwa Libya.
Marshal Khalifa Haftar, kiongozi wa kijeshi Mashariki mwa Libya. Abdullah DOMA / AFP

Wizara ya mambo ya nje ya Urusi, ambayo ilishirikiana na Uturuki kwa kuwakutanisha mahasimu wawili katika mgogoro wa Libya, haikufanikiwa kupata saini ya Marshal Khalifa Haftar kwa makubaliano ya kusitisha mapigano nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Licha ya mazungumzo yaliyodumu saa nane jijini Moscow ambapo Fayez el-Sarraj, kiongozi wa serikali ya Libya yenye makao makuu Tripoli alishiriki, mazungumzo hayakuzaa matunda yoyote.

Mbabe wa kivita Mashariki mwa Libya alikuwa na usiku kucha kuhusu makubaliano hayo. Aliondoka katika mji mkuu wa Urusi bila kusaini makubaliano ya yaliyofikiwa kwa shida Jumatatu alasiri baada ya mazungumzo yaliyodumu saa nane.

Mazungumzo hayo yalianza vibaya, kwani wahusika hao wawili katika mgogoro wa Libya walikataa kuongea ana kwa ana. Hali iliyowalazimu mawaziri wa mambo ya nje wa Urusi na Uturuki kukutana na kila upande ili kurahisisha mambo.

Marshal Khalifa Haftar hakuongea hadharani. Na haijajulikana ni kwa nini alifutilia mbali ya kusitisha mapigano. Lakini kwa mujibu wa vyanzo kadhaa kutoka kambi ya Khalifa Haftar, hatua ya mbabe huyo wa kivita ilisababishwa na jukumu la Uturuki kutamka wazi kwamba yuko tayari kutuma askari nchini Libya kusaidia serikali ya Tripoli inayoongozwa na Fayez el-Sarraj.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.