Pata taarifa kuu
LIBYA-URUSI-UTURUKI-USALAMA-SIASA

Urusi na Uturuki wakutanisha mahasimu wawili Libya

Waziri wa Mambo ya nje wa Uturuki Mevlut Cavusoglu (kushoto) na mwenzake wa Urusi, Sergei Lavrov, katika mkutano wa waandishi wa habari, baada ya kuwakutanisha kwa mazungumzo viongozi wakuu nchini Libya, huko Moscow.
Waziri wa Mambo ya nje wa Uturuki Mevlut Cavusoglu (kushoto) na mwenzake wa Urusi, Sergei Lavrov, katika mkutano wa waandishi wa habari, baada ya kuwakutanisha kwa mazungumzo viongozi wakuu nchini Libya, huko Moscow. © Pavel Golovkin / Pool via REUTERS

Mazungumzo yaliyofanyika Jumatatu wiki hii jijini Moscow kati ya wahusika wakuu katika mzozo wa Libya, kiongozi wa serikali inayotambuliwa na Umoja wa Mataifa, Fayez el-Sarraj, na mbabe wa kivita Mashariki mwa nchi hiyo, Marshal Khalifa Haftar, yamepiga "hatua" bila hata hivyo kufikia makubaliano ya kusitisha vita.

Matangazo ya kibiashara

Baada ya mazungumzo hayo, "hatua kubwa imepigwa", amesema Sergei Lavrov, Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi.

Kiongozi wa serikali inayotambuliwa na Umoja wa Mataifa Fayez al-Sarraj, ametia saini mkataba wa makubaliano ya kusitisha vita, lakini mpizani wake, Khalifa Haftar ameomba muda zaidi kupitia makubaliano hayo

Mbabe huyo wa kivita Mashariki mwa Libya , ametoa muda hadi leo Jumanne asubuhi ili kuweza kutia saini yake kwenye nakal hiyo.

Nakala hiyo inabainisha mfumo wa kusitisha mapigano, mchakato ulioanza kutekelezwa Jumapili, Januari 12.

Hata hivyo mazungumzo hayo yaliyolenga kusaidia kuleta amani na kukomesha mapigano nchini Libya, yameahirishwa baada ya pande pinzani kushindwa kuelewana.

Licha ya Marshal Khalifa Haftar kujizuia kutia saini yake, Sergei Lavrov na mwenzake wa Uturuki, Mevlut Cavusoglu, wamesema wana matumaini kuwa mambo yatakuwa mazuri.

Wakati huo huo Urusi na Uturuki wametoa wito kwa pande zote mbili kukubaliana.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.