Pata taarifa kuu
GAMBIA-SIASA-USALAMA

Gambia yakumbwa na hali ya kutatanisha baada ya maandamano

Waandamanaji wa kundi la "Three Years Jotna" (Miaka Mitatu, muda umewadia) wanadai wanaomba rais Adamu Barrow ajiuzulu, Desemba 16, 2019 Banjul, Gambia. (Picha kumbukumbu).
Waandamanaji wa kundi la "Three Years Jotna" (Miaka Mitatu, muda umewadia) wanadai wanaomba rais Adamu Barrow ajiuzulu, Desemba 16, 2019 Banjul, Gambia. (Picha kumbukumbu). Romain CHANSON / AFP

Gambia inaendelea kukabiliwa na hali ya sintofahamu, baada ya maelfu ya watu kuingia mitaani wakidai rais Adamu Barrow ajiuzulu. Maandamano hayo yalifanyika Jumapili Januari 26 katika mji mkuu wa nchi hiyo Banjul.

Matangazo ya kibiashara

Makabiliano kati ya waandamanaji na polisi yalishuhudiwa. Idadi ya waliopoteza maisha au kujeruhiwa haijajulikana. Wakati huo huo mkurugenzi wa hospitali kuu ya Serrekunda mjini Banjul, Kebbah Manneh, amewaambia waandishi wa habari, ikiwa ni pamoja na wale wa shirika la Habari la AFP kwamba watu watatu walipoteza maisha katika makabiliano hayo. Taarifa ambayo imekanushwa na serikali kupitia msemaji wake, Ebrima Sankareh.

Hali iliendelea kuwa mbaya Jumapili hii Januari 26 katika mji wa Banjul wakati malefu ya waandamanaji walikusanyika kwa wito wa kundi lililoandaa maandamano hayo la "Three Years Jotna", (Miaka mitatu, muda umewadia).

Makabiliano yalizuka wakati waandamanaji ambao walikuwa wanaandamana wakidai rais Adam Barrow ajiuzulu, walitumia barabara nyingine badala ya ile waliokuwa wakitumia awali na kujaribu kukaribia katikati mwa jiji.

Polisi ilitumia gesi ya machozi kuwatawanya waandamanaji, lakini waandamanaji walijibu kwa kutupa mawe.

Serikali imepiga marufuku kundi la "Three Years Jotna" (Miaka mitatu, muda umewadia), kufanya shughuli zozote zile katika ardhi ya Gambia.

Wakati huo huo polisi imemtia nguvuni kiongozi wa kundi hilo Abdou Njie.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.