Pata taarifa kuu
SAHEL-UFARANSA-MAREKANI-USALAMA

Ufaransa yataka Marekani kubaki Sahel

Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa, Florence Parly anazuru WashingtonJanuari 27, 2020 kuzungumza kuhusu muungano unaopambana dhidi ya IS na swala la amani katika Ukanda wa Sahel.
Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa, Florence Parly anazuru WashingtonJanuari 27, 2020 kuzungumza kuhusu muungano unaopambana dhidi ya IS na swala la amani katika Ukanda wa Sahel. REUTERS/Benoit Tessier/File Photo

Waziri wa Majeshi wa Ufaransa Florence Parly anazuru Washington Jumatatu wiki hii kujaribu kuishawishi Marekani isiondoe askari wake katika Ukanda wa Sahel. Msaada wao ni muhimu sana katika kuongoza mapambano dhidi ya makundi ya kijihadi.

Matangazo ya kibiashara

Hivi karibuni Marekani ilitangaza kwamba ina mpango wa kupunguza askari wake katika bara hilo ili kuimarisha vikosi vyake barani Asia. Lakini Ufaransa inataka kufanya kilio chini ya uwezo wake ili Marekani iachane na mpango huo.

Ikiwa kwa wiki kadhaa wanadiplomasia, wanasiasa na wanajeshi wamekuwa wakishughulikia swala hilo katika nyanja zote, Paris inaonekana kuongeza juhudi katika mwezi huu wa Januari.

Jumatatu hii, Waziri wa Majeshi wa Ufaransa, Florence Parly, anatarajia kukutana na Mark Esper, Waziri wa Ulinzi wa Marekani, kabla ya wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa (Quai d'Orsay) kuchukuwa nafasi. Ujumbe kutoka Wizara ya Mambo ya nje ya Ufaransa unatarajia kuzuru Marekani katika siku zijazo.

Januari 13 huko Pau, Emmanuel Macron alisikika akisema, "kuondoka kwa askari wa Marekani itakuwa ni taarifa mbaya."

"Natumai ninaweza kumshawishi rais Trump kwamba mapambano dhidi ya ugaidi pia yanaendelea katika ukanda huo," rais wa Ufaransa alisema.

Marekani ina askari 7,000 waliotumwa barani Afrika, hasa katika Pembe ya Afrika na Niger, na jukulu lao ni muhimu sana kwa kikosi cha askari wa Ufaransa Barkhane.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.