Pata taarifa kuu
LIBYA-AU-UN-USALAMA

Mkutano wa AU kuhusu mgogoro wa Libya kufanyika Alhamisi hii

Rais wa Congo-Brazzaville, Denis Sassou-Nguesso.
Rais wa Congo-Brazzaville, Denis Sassou-Nguesso. EVGENIA NOVOZHENINA / POOL / AFP

Mkutano wa Umoja wa Afrika kuhusu mgpgprp wa Libya unafanyika leo Alhamisi nchini Congo-Brazzaville, baada ya ile iliyofanyika Urusi, Ujerumani na Algeria hivi karibuni.

Matangazo ya kibiashara

Mkutano wa 8 wa Kamati ya ngazi ya juu ya Umoja wa Afrika kuhusu Libya unatarajia kufunguliwa na rais wa Congo-Brazzaville Denis Sassou-Nguesso.

Kulingana na uchunguzi kwamba Umoja wa Mataifa unajitahidi kutoa "suluhisho zenye ushawishi mkubwa" kwa pande husika na kwamba "hali inazidi kuwa mbaya", Umoja wa Afrika sasa unataka kuchukua jukumu la kusuluhisha mzozo wa Libya.

Mkutano ambao unafanyika Alhamisi hii huko Brazzaville unalenga "kuwashawishi wahusika wa mzozo huo kukubali wazo la kuandaa mkutano wa maridhiano".

Taarifa ya mwisho iliyopitishwa mwishoni mwa mkutano wa hivi majuzi huko Berlin inataja mkutano huo wa baadaye, ambao unapaswa kufanyika huko Addis Ababa miezi sita ijayo.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.