Pata taarifa kuu
DRC-USALAMA

Mkuu wa zamani wa idara ya ujasusi DRC azuiliwa kwa muda wa saa kadhaa

Afisa wa zamani wa idara ya ujasusi DRC (ANR) alikamatwa wakati akishuka kwenye ndege, kisha kupelekwa makao makuu ya ANR katikati mwa jiji la Kinshasa (picha ya kumbulumbu).
Afisa wa zamani wa idara ya ujasusi DRC (ANR) alikamatwa wakati akishuka kwenye ndege, kisha kupelekwa makao makuu ya ANR katikati mwa jiji la Kinshasa (picha ya kumbulumbu). Photo by Ute Grabowsky/Photothek via Getty Images

Mkuu wa zamani wa idara ya ujasusi nchini DRC (ANR) Kalev Mutondo, amezuiliwa kwa saa kadhaa baada ya kukamatwa Jumatano hii Februari 12 katika uwanja wa ndege wa Kinshasa.

Matangazo ya kibiashara

Kalev Mutondo alihojiwa kwa masaa kadhaa na maafisa wenzake wa zamani. Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa, Kalev Mutondo alizuiliwa kutokana na mambo yanayaohusiana na usalama.

Afisa mwandamizi wa idara ya ujasusi nchini DRC amethibitisha kukamatwa kwa Kalev Mutondo Jumatano alasiri wakati akishuka kwenye ndege na saa chache baadaye alipelekwa makao makuu ya idara hiyo, katikati mwa jiji la Kinshasa kwa mahojiano.

Mwanzoni mwa mahojiano, Kalev Mutondo, ambaye alikuwa na simu zake mbili, alionekana akijibu simu kutoka kwa watu mbalimbali, akikana kukamatwa kwake na kudai kwamba labda alikuwa ametulia nyumbani kwake, au kwamba alikuwa amekwenda makao makuu ya idara ya ujasusi (ANR) kumtembelea naibu wake wa zamani ambaye amekuwa mkuu wa idara hiyo.

Maafisa waliokuwa wanamhoji waliamua kukamata simu zake hadi mwisho wa mahojiano, karibu saa moja usiku, aliporuhusiwa kwenda nyumbani.

Kuhusu kesi hiyo, idara ya ujasusi, sawa na Kalev Mutondo, wameamua kusalia kimya. Kulingana na vyanzo vyetu, mkuu huyo wa zamani wa ANR anatuhumiwa kuwa yuko miongoni mwa watu wanaotaka kuzorotesha shughuli za utawala mpya mjini Kinshasa. Mpango uliofichuliwa wakati wa safari yake ya mwisho kwenda Uganda. Kalev Mutondo kwa sasa yuko chini ya uangalizi wa idara ya ujasusi "wakati wowote atakapohitajika," kimesema chanzo kilicho karibu na uchunguzi.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.