Pata taarifa kuu
LIBYA-USALAMA

Vikosi vya Haftar vyapiga marufuku safari za ndege za Umoja wa Mataifa kwenda Tripoli

Marshal Khalifa Haftar, mbabe wa kivita Mashariki mwa Libya.
Marshal Khalifa Haftar, mbabe wa kivita Mashariki mwa Libya. Abdullah DOMA / AFP

Vikosi vya Marshal Khalifa Haftar, ambavyo vinadhibiti Mashariki mwa Libya, haviruhusu tena Umoja wa Mataifa kutumia uwanja wa ndege wa Tripoli, mmoja wa wasemaji wa vikosi hivyo amesema.

Matangazo ya kibiashara

Umoja wa Mataifa utalazimika kutumia viwanja vingine vya ndege, kama ule wa Misrata, kwa sababu vikosi vya ANL vya Marshal Haftar haviwezi kuhakikisha usalama wa ndege kwenye uwanja wa ndege wa Mitiga wa Tripoli ambao Uturuki imeufanya kuwa kambi yake ya jeshi, Ahmed Mismari amewaambia waandishi wa habari huko Benghazi, mji wa kwanza kwa ukubwa Mashariki mwa Libya.

Tangu mwezi Aprili vikosi vya ANL vimekuwa vikitafuta kudhibiti mji wa Tripoli bila mafanikio. Mji wa Tripoli ni makao makuu ya serikali ya umoja wa kitaifa inayoongowza na Fayez al Sarraj, serikali ambayo inatambuliwa na jamii ya kimataifa.

Hata hivyo ANL ina uwezo mkubwa kwa vita vya anga kutokana na ndege zisizo na rubani inayopewa na Falme za Kiarabu, ambazo zinapaa eneo lote la Libya kupitia mawasiliano ya satelaiti, kulingana na ripoti ya UN iliyochapishwa mwezi Novemba.

Uturuki, ambayo inasaidia serikali ya umoja wa kitaifa, imeipa Tripoli ndege zisizo kuwa na rubani na mifumo ya juu ya ulinzi wa ndege katika mji mkuu Tripoli.

Siku ya Jumatano, Umoja wa Mataifa ilionya kwamba vizuizi vya ndege vilivyowekwa na ANL vinaweza kutatiza juhudi za kibinadamu na upatanishi nchini Libya, inayokumbwa na machafuko tangu kupinduliwa kwa Muammar Gaddafi mwaka 2011.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.