Pata taarifa kuu
DRC-AJALI-KINSHASA-MAAFA

DRC: Maafa jijini Kinshasa baada ya Lori kugonga magari na pikipiki

Ajali ya barabarani jijini Kinshasa, Februari 16 2020
Ajali ya barabarani jijini Kinshasa, Februari 16 2020 Droits tiers.

Watu wengi wanahofiwa kupoteza maisha na wengine kujeruhiwa baada ya kutokea kwa ajali ya barabarani jijini Kinshasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo siku ya Jumapili mchana.

Matangazo ya kibiashara

Uongozi wa jiji hilo umethibitisha kutokea kwa ajali hiyom katika mzunguko wa barabara hiyo kwenda Chuo Kikuu cha Kinshasa, na inahofiwa kuwa idadi ya watu waliopoteza maisha, itaongezeka.

Ripoti za awali zinaseema kuwa watu zaidi ya 10 ndio waliopoteza maisha kufikia Jumapili jioni.

Walioshuhudia ajali hiyo wanasema, ajali hiyo ilitokea katika eneo la Nigaba  baada ya Lori lililokuwa limebeba mawe kugonga magari yaliyokuwa na abiria, pikipiki na watu waliokuwa wanatembea kwa miguu.

Joseph Enenge Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kinshasa, ameiambia Radio Okapi kuwa, breki za lori hilo zilikatika kabla ya kupoteza mwelekeo na kugonga magari hayo.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.