Pata taarifa kuu
LIBYA-UN-VITA-AMANI

Umoja wa Mataifa wasema hali nchini Libya inaendelea kuwa mbaya

Mwanajeshi wa serikali ya Libya, akiwa tayari kwa vita karibu na jiji kuu Tripoli kupambana na vikosi vya upinzani
Mwanajeshi wa serikali ya Libya, akiwa tayari kwa vita karibu na jiji kuu Tripoli kupambana na vikosi vya upinzani ©REUTERS/Ismail Zitouny

Umoja wa Mataifa unasema hali ya nchi ya Libya inaendelea kuwa mbaya kila siku huku mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini humo Stephanie Williams akisema kuwa maelewano ya kusitisha mapigano, hayajaheshimiwa.

Matangazo ya kibiashara

Wakati uo huo, Kiongozi wa serikali inayotambuliwa na Umoja wa MataifaFayez al-Sarraj, ameonya kuwa, hatua ya baadhi ya mataifa ya Magharibi kuendelea kumuunga mkono Jenerali Khalifa Haftar anayeongoza vikosi vya upinzani, itaendeleza mzozo nchini humo.

Sarraj ameongeza kuwa, iwapo uungwaji mkono hjuo utaendelea, utajenga chuki miongoni mwa raia wa nchi hiyo, suala ambalo litakuwa gumu kulimaliza.

Aidha, amemtaja Haftar ambaye vikosi vyake vinaendeleza mapigano kudhibiti jiji kuu Tripoli, kama mshirika mbaya asiyeweza kusaidia kuleta amani katika taifa hilo la Afrika Kaskazini.

Juhudi za kuleta amani nchini humo kupitia mazungumzo ya amani ambayo yamekuwa yakiendelea huko Geneve, hayajazaa matunda.

 

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.