Pata taarifa kuu
LIBYA-USALAMA-SIASA

Libya GNA yasitisha ushiriki wake katika mazunguzo ya Geneva

Waziri Mkuu wa Libya Fayez al-Sarra jhuko Tripoli, Novemba 8, 2018.
Waziri Mkuu wa Libya Fayez al-Sarra jhuko Tripoli, Novemba 8, 2018. AFP

Serikali ya umoja wa kitaifa nchini Libya (GNA) yenye makao yake makuu Tripoli, inayotambuliwa na Umoja wa Mataifa, imetangaza usiku wa tarehe 18 kuamkia 19 Februari kwamba imesitisha ushiriki wake katika mazungumzo yaliyo kuwa yakiendelea huko Geneva.

Matangazo ya kibiashara

GNA inasema imechukuwa uamuzi huo kutokana na ukiukwaji wa mara kwa mara wa makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyofikiwa tangu mwezi Januari.

Serikali ya umoja wa kitaifa (GNA) ya Waziri Mkuu Fayez el-Sarraj imebaini katika taarifa kwamba inajiondoa katika mazungumzo hayo ya amani huko Geneva hadi pale kutapitishwa "hatua dhidi ya mvamizi", Khalifa Haftar ambaye askari wake wamekuwa wakijaribu kuchukua udhibiti wa Tripoli tangu mwezi Aprili mwaka jana.

GNA inashutumu vikosi vya waasi kwa kukiuka mara kwa mara makubaliano ya kiusitisha mapigano yaliyofikiwa tangu mwezi uliopita. Makabiliano ya mwisho yalitokea Februari 18 alaasiri wakati makombora karibu kumi na tano yalipoanguka kwenye bandari za Tripoli na Al-Chaab.

Raia watatu waliuawa na wengine watano kujeruhiwa, kwa mujibu wa msemaji wa wizara ya afya ya Libya, Amine al-Hachemi.

Mazungumzo ya amani yaliyokuwa yakifanyika huko Geneva, Uswisi, kwa sasa, yamesitishwa.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.