Pata taarifa kuu
SOMALIA-KENYA-AL SHABAB-USALAMA

Al Shabab yatekeleza mashambulio matatu nchini Kenya na Somalia

Afisa wa polisi wa Somalia akiwa karibu na mabaki ya gari lililoharibiwa na mlipuko wa bomu uliotekelezwa na wanamgambo wa Kiislamu wa Al Shabab, mbele ya idara inayohusika na masuala ya uchunguzi wa makosa ya jinai huko Mogadishu, Julai 31, 2016.
Afisa wa polisi wa Somalia akiwa karibu na mabaki ya gari lililoharibiwa na mlipuko wa bomu uliotekelezwa na wanamgambo wa Kiislamu wa Al Shabab, mbele ya idara inayohusika na masuala ya uchunguzi wa makosa ya jinai huko Mogadishu, Julai 31, 2016. REUTERS/Ismail Taxta

Wanamgambo wa Al Shabab kutoka Somalia wametekeleza mashambulio mawili dhidi ya kambi kadhaa za kijeshi huko Qoryoley, kilomita thelathini Magharibi mwa Mogadishu.

Matangazo ya kibiashara

Idadi ya watu waliouawa katika mashambulizi hayo haijajulikana.

Silaha kadhaa ziliibwa, kulingana na vyanzo kadhaa kutoka Somalia.

Shambulio la pili lilitokea saa chache baada ya shambulio la kwanza dhidi ya kabimbi nyingine ya jeshi katika mazingira yanayofanana, huko Ceel-Salini, kilomita thelathini kutoka eneo ambalo kumetokea shambulizi la kwanza.

Afisa katika jeshi la Somalia ameliambia shirika la Habari la AFP kwamba washambuliaji hao walitimiliwa kwa msaada wa kikosi cha jeshi la Umoja wa Afrika nchini Somalia, AMISOM.

Wanamgambo hao pia wametekeleza shambulizi jingine baya dhidi ya basi la abiria lililokuwa likitokea Mandera likielekea Nairobi nchini Kenya.

Abiria watatu waliuawa katika shambulio hilo la kushtukiza.

Tangu mwanzoni mwa mwaka huu, wanamgambo wakiislamu wa kundi la Al Shabab wameongeza mashambulizi mbali na mpaka wa Somalia katika juhudi za kuonyesha kuwa bado wana nguvu katika ukanda huo, pamoja na Januari 5 dhidi ya jeshi la Marekani, na kuapa kwamba Kenya "haitakuwa kamwe na usalama ".

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.