Pata taarifa kuu
LESOTHO-SIASA-HAKI

Waziri Mkuu wa Lesotho kushtakiwa kwa mauaji ya mke wake wa zamani

Waziri Mkuu Thomas Thabane atafikishwa mahakamani Ijumaa, hii Februari 21, katika kesi mauaji ya mke wake wa zamani (picha ya kumbukumbu).
Waziri Mkuu Thomas Thabane atafikishwa mahakamani Ijumaa, hii Februari 21, katika kesi mauaji ya mke wake wa zamani (picha ya kumbukumbu). GIANLUIGI GUERCIA / AFP

Waziri Mkuu wa Lesotho Thomas Thabane anatarajiwa kufikishwa mbele ya mahakama Ijumaa hii Februari 21. Kulingana na vyanzo vya polisi, hatma yake tayari inajulikana: atashtakiwa rasmi kwa mauaji ya mke wake wa zamani. Uchunguzi ulikuwa umesitishwa kwa miaka miwili.

Matangazo ya kibiashara

Lipolelo Thabane, 58, aliuawa Juni 14, 2017 alipokuwa anarudi nyumbani kwa gari huko Maseru, mji mkuu wa Lesotho. Siku mbili baadaye, mumewe, Thomas Thabane aliteuliwa rasmi kuwa Waziri Mkuu wa Lesotho.

Siku chache baadaye Thomas Thabane alionekana akifuatana kimapenzi na Maesaiah, ambaye baadaye alimuoa na kuwa mke wake wa pili.

Uchunguzi kuhusu mauaji ya Lipolelo Thabane ulisitishwa kwa kipindi cha miaka mbili. Mapema mwezi Februari 2020, mke mpya wa Waziri Mkuu alishtakiwa rasmi kwa mauaji ya mke mwenza. Ijumaa wiki hii ni zamu ya Waziri Mkuu Thomas Thabane kusikilizwa kuhusu mauaji hayo.

Waziri Mkuu mwenye umri wa miaka 80 anatarajiwa kushtakiwa rasmi kwa mauaji ya mke wake wa kwanza. "Hii ndio ilikubaliwa na wakili wake," Naibu mkuu wa polisi ameliambia shirika la Habari la AFP. "Hii haimaanishi kuwa alikuwepo katika eneo la uhalifu, lakini kwamba alitenda kwa kushirikiana na wauaji (wahusika), " amesema afisa huyo wa polisi.

Ni kwa muktadha huu Waziri Mkuu Thomas Thabane alitangaza Alhamisi kwamba ataachia ngazi mwishoni mwa Julai. Chama chake, cha ABC (All Basotho Convention), amabacho kinabaini kwamba kimechoshwa na kesi, pia kimeapa kumtimua haraka iwezekanavyo waziri huyo mkuu kwenye nafasi yake.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.