Pata taarifa kuu
MALI-USALAMA

Mali: Askari wasiopungua 3 wauawa katika shambulio dhidi ya kambi ya jeshi ya Bambara Maoudé

"Kikosi cha wanajeshi wa Mali (FAMA) huko Bambara Maoudé, karibu kilomita 100 Kusini mwa Timbuktu," kilishambuliwa na magaidi karibu saa 5:00 asubuhi, " jeshi la Mali liliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter.
"Kikosi cha wanajeshi wa Mali (FAMA) huko Bambara Maoudé, karibu kilomita 100 Kusini mwa Timbuktu," kilishambuliwa na magaidi karibu saa 5:00 asubuhi, " jeshi la Mali liliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter. Google Maps

Mali inaendelea kukumbwa na mashambulizi ya hapa na pale, huku vikosi vya usalama na ulinzi ndio vikilengwa zaidi katika mashambulizi hayo. Makundi ya wanamgambo wa Kiislamu yananyooshewa kidole kuhusika na mashambulizi hayo.

Matangazo ya kibiashara

Wanajeshi watatu wa Mali wameuawa na watano kujeruhiwa wakati wa shambulio dhidi ya kambi ya jeshi huko Bambara Maoudé, katika mkoa wa Timbuktu, Kaskazini mwa Mali.

Shambulio hilo lililitekelezwa Jumapili Februari 23 na watu wanaodaiwa kuwa wanamgambo wa Kiislamu nchini humo.

Shambulio hilo lilitokea katika eneo la Bambara Maoudé kilomita mia moja kutoka Timbuktu.

Washambuliaji wanaodaiwa kuwa wanamgambo wa Kiislamu walitumia pikipiki, na magari yenye nembo za jeshi la Mali, FAMA, kwa kuweza kuingia katika kambi hiyo.

Askari watatu waliuawa, wengine walijeruhiwa, lakini miili ya asjari hao na wale waliojeruhiwa walipelekwa baadae katikati mwa Mali kwa helikopta yatume ya Umoja wa mataifa nchini Mali.

Vifaa kadhaa vya jeshi viliporwa na washambuliaji. Kwa upande wao, washambuliaji kadhaa waliuawa, kwa mujibu wa chanzo kutoja jeshi la Mali.

Baada ya shambulio hilo jipya, wataalam wanaona kwamba washambuliaji wamekuwa na tabia ya kujifananisha na vikosi vya serikali.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.