Pata taarifa kuu
TOGO-UCHAGUZI-SIASA

Togo: CENI yamtangaza Faure Gnassingbé mshindi katika uchaguzi wa urais

Mwenyekiti wa CENI Tchambakou Ayassor (wa pili kutoka kulia), akiwa amezungukwa na wajumbe wengine wa tume hiyo, akitangaza matokeo ya uchaguzi wa urais nchini Togo huko Lomé, Februari 24, 2020.
Mwenyekiti wa CENI Tchambakou Ayassor (wa pili kutoka kulia), akiwa amezungukwa na wajumbe wengine wa tume hiyo, akitangaza matokeo ya uchaguzi wa urais nchini Togo huko Lomé, Februari 24, 2020. PIUS UTOMI EKPEI / AFP

Kulingana na matokeo rasmi ya awali yaliyotangazwa usiku wa Jumapili kuamkia leo Jumatatu na Tume huru ya taifa ya uchaguzi, Faure Gnassingbé amechaguliwa tena kwa muhula wa nne kama rais wa Togo.

Matangazo ya kibiashara

"Kulingana na matokeo yote yaliyohesabiwa, mgombea wa chama cha UNIR, Bwana Gnassingbé Essozimna Faure ametangazwa kuwa rais wa Jamhuri ya Togo", ametangaza Tchambakou Ayassor, Mwenyekiti wa Tume huru ya taifa ya uchaguzi, baada ya kupinga matokeo ya ofisi 46 za tume ya uchaguzi katika mae,neo mbalimbali nchini humo.

Kulingana na takwimu kutoka CENI, Faure Gnassingbé amechaguliwa tena katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais kwa asilimia 72.36 ya kura, sawa na karibu alama zaidi ya 14 wakati alipochaguliwa kama rais wa Togo mwishoni mwa mwaka 2015. Kiwango cha ushiriki kilifikia 76 , 63%, pia kiwango kikubwa zaidi kuliko mwaka wa 2015 wakati ambapo kiwango cha ushiriki kilifikia 61%.

Upande wa upinzani, Waziri Mkuu wa zamani na mpinzani mkuu wa Bw Gnassingbé, Agbéyomé Kodjo almepata asilimia 18.37 ya kura. Kiongozi wa ANC, Jean-Pierre Fabre anachukuwa nafasi ya tatu kwa asilimia 4.35. Ni mara ya kwanza Tume huru ya kitaifa ya uchaguzi kutangaza haraka matokeo ya uchaguzi wa urais. Matokeo haya yatapelekwa kwenye Mahakama ya Katiba, ambayo ina siku sita ya kuuchunguza na kutangaza matokeo ya mwisho.

"Ni kweli kabisa," Waziri wa Wafanyakazi wa serikali Gilbert Bawara, mshirika wa karibu wa rais Gnassingbé.

Kwenye akaunti yake ya Twitter, Faure Gnassingbé ameshukuru "vijana wa Togo ambao wametakiwa kusherehekea ushindi huo kwa niaba ya demokrasia. "

Lakini matokeo haya tayari yamepingwa. Mashirika ya kiraia yamegundua visanduku vya kura ambavyo vilijazwa kura kabla ya uchaguzi na kubaini kwamba matokeo ya uchaguzi yamebadilishwa. Tangu Jumamosi jioni, Agbéyomé Kodjo ameshtumu kuwepo na "udanganyifu mkubwa" katika uchaguzi huo.

Na hata kabla ya kutangazwa kwa matokeo ya urais na CENI, Agbéyomé Kodjo alifanya mkutano na waandishi wa habari jijini Lomé, akithibitisha kwamba kulingana na takwimu alizo nazo, bila shaka yeye ndio mshindi wa uchaguzi.

Hata hivyo Agbéyomé Kodjo amemtaka Faure Gnassingbé kukubali kushindwa.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.