Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-CORNA-AFYA

Coronavirus-Bukina Faso: Wafungwa 1,200 waachiliwa huru kwa msamaha wa rais

Rais wa Burkina FasoRoch Marc Christian Kabore.
Rais wa Burkina FasoRoch Marc Christian Kabore. LUDOVIC MARIN / POOL / AFP

Rais wa Burkina Faso Roch March Christian Kabore amewaachia huru wafungwa 1,200 ikiwa ni mojawapo ya mikakati ya kupambana na virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19.

Matangazo ya kibiashara

Wafungwa hao walisamehewa kwa misingi ya umri wao mkubwa, hali zao za kiafya na wale waliokuwa wametumikia vifungo vyao kwa muda mrefu.

Rais Kabore ameahidi kutoa vyakula pamoja na mahitaji muhimu kwa watu wasiojiweza katika kipindi hiki.

Zaidi ya watu milioni tano kutoka ukanda wa Sahel wanakabiliwa na baa la njaa kutokana na mlipuko wa Corona, limesema shirika la mpango wa chakulu duniani, WFP.

WFP kwenye taarifa yake imesema mataifa yaliyo na hali tete ni Burkina Faso, Mali na Niger.

Wakati huo huo shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu Amnesty International,  limekosoa namna ambavyo polisi nchini Nigeria wanavyotumia nguvu kupita kiasi kutekeleza marufuku ya kutotembea nchini humo katika vita dhidi ya Corona.

Mikanda ya Video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii  inaonesha namna wananchi wanachapwa na polisi.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.