Pata taarifa kuu
AFRIKA-CHINA-CORONA-AFYA

Viongozi wa Afrika waendelea kuinyooshea kidole cha lawama China

Raia wa Kiafrika katika eneo la "Little Africa" huko Guangzhou (Canton), Machi 2, 2018.
Raia wa Kiafrika katika eneo la "Little Africa" huko Guangzhou (Canton), Machi 2, 2018. Fred DUFOUR / AFP

Viongozi wa mataifa ya Afrika wameendelea kuonesha gadhabu zao kufuatia visa vya kuendelea kuteswa na kubaguliwa kwa Waafrika nchini China kwa madai kuwa wanasambaza virusi vya Corona.

Matangazo ya kibiashara

Waafrika wanaoishi katika miji mbalimbali nchini China hasa katika mji wa Guangzhou wameendelea kulalamika kuondolewa makwao kwa nguvu, kubaguliwa wanapokwenda madukani na mikahawani huku wakilazimishwa kufanyiwa vipimo vya mamaambukizi ya Virusio vya Corona.

Umoja wa Afrika umeonesha masikitiko yake na kuitaka serikali ya China kuchukua hatua ya kusitisha uteswaji wa Waafrika katika taifa hilo la bara Asia.

Hivi karibuni, Mabalozi wa mataifa ya Afrika wapatao 20 waliandikia baruia serikali ya China kulalamilikia mateso  hayo ambayo wanasema ni ya kibaguzi.

Uongozi wa mji wa Guangzhou, amnbao una watu Milioni 15 unajitetea kuwa; hatia ya maafisa wake ni kupambana na vurusi vya Corona, wakati huu Beijing ikisema maambukizi mapya yanatoka nje ya nchi hiyo.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.