Pata taarifa kuu
DRC-EBOLA-AFYA

DRC: Mgonjwa wa Ebola atoroka, hofu ya kuonea kwa maambukizi zaidi yatanda Beni

Mnamo tarehe 4 ya mwezi Machi mwaka huu wa 2020, WHO ilikuwa iliyooiita habari njema kuwa mgonjwa wa mwisho wa Ebola nchini DRC ameruhiswa kurejea nyumbani baada ya kupatiwa matibabu katika kituo cha matibabu huko kaskazini mashariki mwa mji wa Beni
Mnamo tarehe 4 ya mwezi Machi mwaka huu wa 2020, WHO ilikuwa iliyooiita habari njema kuwa mgonjwa wa mwisho wa Ebola nchini DRC ameruhiswa kurejea nyumbani baada ya kupatiwa matibabu katika kituo cha matibabu huko kaskazini mashariki mwa mji wa Beni REUTERS/Goran Tomasevic/File Photo

Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema lina hofu ya kuzuka upya kwa maambukizi ya virusi vya Ebola Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo baada ya kutoroka kwa mgonjwa wa Ebola katika kituo kinachotoa huduma za wagonjwa wa virusi hivyo.

Matangazo ya kibiashara

Siku zilizopita Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ilitangaza kumalizika kwa mlipuko wa ugonjwa hatari wa Ebola ulioikumba mara mbili nchi hiyo, baada ya maambukizi mapya kugundulika Aprili 10 mwaka huu, baada ya kutoripotiwa kisa chochote cha virusi hivyo kwa wiki zaidi ya saba.

Tangu wakati huo maafisa wa afya wanajaribu kudhibiti maambukizi yoyote mapya yanayoweza kuzuka.

Siku ya Ijumaa, dereva wa pikipiki ya kukodiwa, mwenye umri wa miaka 28, aliyepatikana na virusi vya Ebola alitoroka kituo ambako alikuwa akipewa huduma za matibabu katika mji wa Beni.

"Hatuna maelezo bado (...) Zoezi la kumtafuta linaendelea," amesema Boubacar Diallo, afisa wa WHO.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.