Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-CORONA-UCHUMI

Ramaphosa atangaza mpango wa matumizi ya mabilioni ya fedha kudhibiti mgogoro wa kiuchumi

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa akilihutubia Taifa huko Cape Town Februari 13, 2020.
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa akilihutubia Taifa huko Cape Town Februari 13, 2020. REUTERS/Sumaya Hisham/File Photo

Wakati raia nchini Afrika Kusini wametakiwa kuendendelea kusalia makwao hadi Mei 1, marufu hiyo ya kutotembea imezua sintofahamu nchini humo. Katika vitongoji duni, watu wanakabiliwa na njaa na hali hiyo inayowakabili imesababisha vurugu na uporaji.

Matangazo ya kibiashara

Kutokana na hali hiyo Rais Cyril Ramaphosa ameamua kutangaza mfululizo wa hatua za kiuchumi.

Hali inazidi kuwa mbaya katika vitongoji duni, kwani nchi hiyo sasa imeingia wiki yake ya nne ya marufuku ya kutotembea. Nchini Afrika Kusini kunaripotiwa visa 3,465 vya maambukizi ya virusi vya Corona yaliyothibitishwa, na watu 58 wameuawa kwa ugonjwa huo.

Wakazi wa vitongoji hivyo duni wamejawa na hasira, wakati wengi wao hawana chakula. Maandamano yameongezeka katika siku za hivi karibuni katika maeneo haya masikini, na kusababisha mara nyingi makabiliano na polisi.

Visa vya uporaji pia vimeongezeka katika eneo lilokaribu na Cape Town: Jumatatu wiki hii, malori mawili yaliyokuwa yamesheheni chakula yalishambuliwa na kuibiwa. Jana Jumanne, maduka ya jumla ya chakula yalilengwa katika eneo la Macassar, mashariki mwa Cape Town.

Kwa kujibu matatizo hayo ya kijamii, Rais Cyril Ramaphosa ametangaza mpango wa hatua za kiuchumi za Euro bilioni 24, ambapo Euro bilioni 2.5 zitatumika kwa kuongeza misaada ya kijamii, kwa miezi ijayo.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.