Pata taarifa kuu
BURUNDI

Kampeni zaendelea nchini Burundi licha ya tishio la Covid 19

Nchi ya Burundi yazindua kampeni za uchaguzi mkuu licha ya hofu ya Corona
Nchi ya Burundi yazindua kampeni za uchaguzi mkuu licha ya hofu ya Corona The Independent Uganda

Nchini Burundi kampeni za uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika  tarehe 20 ya mwezi ujao zimeendelea, ambapo  Jumla wagombea 7 wanawania kiti cha urais wakiwemo wagombea huru 2.

Matangazo ya kibiashara

Miongoni mwa wagombea urais kuwa saba, wawili pekee ndio wanapewa bahati ya kuweza kuibuka washindi ambapo ni  pamoja na mpinzani mashuhuri Agathon Rwasa wa chama CNL pamoja na Evariste NDAYISHIMIYE wa chama tawala CNDD-FDD.

Akizindua kampeni zake mjini Ngozi kaskazini mwa nchi kwenye siku ya kwanza ya kampeni zake Agathon RWASA alikosoa sera za serikali ya sasa na kueleza kuwa yeye ndoto yake ni kuijenga Burundi yenye haki kwa wote.

Upande wake Evariste NDAYISHIMIYE, mgombea wa chama CNDD-FDD, ambaye alizindua kampeni zake mkoani Gitega katikati mwa nchi amesema kipaumbele chake kitakuwa kuinuwa sekta za uzalishaji.

Uchaguzi wa Mei 20 utajumuisha chaguzi tatu kwa mpigo ikiwa ni pamoja na uchaguzi wa urais, uchaguzi wa wabunge na ule wa madiwani.

Hata hivyo kampeni hizi zinafanyika katika hali ya kutatanisha kiafya kutokana na janga la ugonjwa wa Covid-19 baadhi wakihofia kutokea ongezeko la visa vya maambukizi kutokana na msongamano wa watu kwenye kampeni hizi.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.