Pata taarifa kuu
MALI-USALAMA

Mali: Kijiji cha Boulikessi chaendelea kukumbwa na machafuko ya mara kwa mara

Vijana wakionyeshwa kama wanajihadi wa zamani (picha ya kumbukumbu).
Vijana wakionyeshwa kama wanajihadi wa zamani (picha ya kumbukumbu). RFI/Coralie Pierret

Mkuu wa kijiji cha Boulikessi nchini Mali hajulikani aliko baada ya taarifa za kutoweka kwake Jumanne Mei 19 karibu na eneo la mipaka mitatu kati ya Mali, Burkina Faso na Niger.

Matangazo ya kibiashara

Kwa miaka miwili sasa, kijiji hiki maarufu, kinaendelea kukumbwa na machafuko yanayoendeshwa na makundi ya kijihadi, lakini pia na wanajeshi.

Tangu kuondoka kwake kuhudhuria uzinduzi wa maonyesho ya Hombori, Hama Abdou Diallo hajarudi tena nyumbani kwake, mmoja wa ndugu zake amesema.

Jumanne asubuhi wiki hii, kaimu mkuu wa kijiji cha Boulikessi aliondoka nyumbani kwake kwa baiskeli, baada ya kutembea kilomita 75 kutoka nyumbani kwake alitekwa nyara na kundi la watu wasiojulikana, hadi leo hajarudi.

Hama Abdou Diallo alikuwa akikaimu nafasi hiyo, kwa sababu mkuu wa kijiji cha Boulikessi, Amirou Boulikessi, alitekwa nyara Machi 13, 2019 na kundi la wanajihadi, kulingana ushuhuda unaotolewa na ndugu zake.

Hadi leo, Amirou Boulikessi bado hajapatikana. Katika kipindi cha mwaka mmoja, kijiji cha Boulikessi kimewapoteza viongozi wake wawili. Kijiji hiki ambacho kinappatikana karibu na kijiji cha Mondoro kwenye mpaka na Burkina Faso kinakabiliwa na mashambulizi ya mara kwa mara ya makundi ya kijihadi.

Wakati huo huo jeshi la Mali limeendelea kunyooshewa kidole cha lawama na tume ya Umoja wa Mataifa nchini humo kwa kuhusika na ukiukwaji wa haki za binadamu.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.