Pata taarifa kuu
AFRIKA MASHARIKI-MAJANGA ASILI

Nzige wa jangwani, Covid-19 na mafuriko: Afrika Mashariki yakabiliwa na migogoro mitatu mfululizo

Kenya, Februari 2020, mkulima huyu akiwafukuza nzige wa jangwani waliovamia shamba lake, karibu na Nanyuki (Kaunti ya Laikipia).
Kenya, Februari 2020, mkulima huyu akiwafukuza nzige wa jangwani waliovamia shamba lake, karibu na Nanyuki (Kaunti ya Laikipia). REUTERS/Baz Ratner

Benki ya Dunia imetoa kitita cha dola milioni 500 kupambana na nzige wa jangwani. Pesa hizo zitatumika sana katika ukanda wa Afrika Mashariki, uliovamiwa na wadudu hatari.

Matangazo ya kibiashara

Ukanda huo kwa sasa uko katika hali ya sintofahamu, kwani nzige wa jangwani wanakuja kuongeza hali nzito ya kibinadamu kutokana na migogoro inayo ukumba kwa sasa.

Methali hii "penye tatizo hapakosi lingine" imeuvaa ukanda wa Afrika Mashariki mwaka huu. Kufuatia mvua za kubwa, ukanda huu unaendelea kushuhudia maeneo kadhaa ya kuvamiwa na nzige wa jangwani baada ya miaka 70.

Pesa kutoka Benki ya Dunia zitakwenda moja kwa moja kwa familia, wafugaji, wakulima, zitatumika katika ununuzi wa mbolea na mbegu, na ufadhili wa mifumo ya ufuatiliaji na tahadhari.

Cyril Ferrand wa shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula FAO ameeleza kuwa ana "wasiwasi na mvua ambazo zimeanza tena kujikusanya, na hivyo kusababisha kitisho hatari kwa usalama wa chakula".

Kwa uhakika, pamoja na mvua, mazao yaliyo karibu na kukua yatalazimika kumezwa na wadudu. Mvua ambazo zimesababisha mamia ya vifo, na mafuriko, maporomoko ya ardhi, na uharibifu wa kila aina. Ziwa Victoria, kwa mfano, kimefikia kiwango ambacho hakijawahi kuonekana.

Hali kwa kweli sio nzuri, kwani mvua zimesababisha janga la kipindupindu nchini Kenya, na sasa nchi hiyo imerekodi zaidi ya wagonjwa 500, kwa mujibu wa FAO.

Haya yanajiri wakato ugonjwa unaosababishwa na virusi vya Corona, Covid-19, unaendelea kuathiri vibaya uchumi ambao ni dhaifu na na kusababisha mgogoro wa kiafya.

Mfano nchini Sudani Kusini, ambapo baada ya mauaji ya kikabila na mamia ya vifo mwishoni mwa wiki iliyopita, shirika la Msalaba na Mwezi Mwekundu, ICRC, linasema ni linapata shida kutoa msaada kwa raia kwa sababu ya vizuizi vilivyowekwa kutokana na Corona. Hii inamaanisha ugumu wa usafiri, kutembea kutoka eneo moja kwenda eneo jingine na kupunguzwa kwa idadi ya vitanda. Shirika hilo linatabiri kutokea kwa vifo vingi zaidi kwani watu waliojeruhiwa hawawezi kutibiwa.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.