Pata taarifa kuu
CHINA-JAPANI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Maambukizi mapya ya virusi vya Covid-19 yapungua China

Nchini China, raia waendelea kukabiliana na maambukizi ya virusi vya ugonjwa hatari wa Covid-19 (Corona).
Nchini China, raia waendelea kukabiliana na maambukizi ya virusi vya ugonjwa hatari wa Covid-19 (Corona). Reuters/Li Wenliang

China imetangaza kwamba maambukizi ya virusi vya ugonjwa unaofahamika sasa kama Covid-19 au Corona yamepungua kwa kiwango kikubwa. Lakini maafisa na wachambuzi wameaonya kuwa kitisho za virusi hivyo bado kipo.

Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo nchini Japani, hali bado ni ngumu baada ya kuripotiwa vifo vya watu wawili walioambikizwa virusi hivyo waliokwama katika meli ya Diamond Princess, iliyowekwa karantini kwenye pwani ya Yokohama, nchini humo.

Tume ya kitaifa (Wizara) ya Afya imeripoti vifo vya watu 114 walioambukizwa virusi vya ugonjwa wa Covid-19 nchini China ndani ya muda wa saa 24, na kusababisha idadi ya vifo kote nchini humo (ukiondoa Hong Kong na Macao) kufikia 2,118.

Lakini imetangaza kesi mpya 394 za maambikizi ya virusi vya Covid-19, ishara kwamba sasa maambukizi hayo yameanza kupunguwa kwa kiwango cha kuridhisha, imesema Wizara ya Afya ya China.

Kwa jumla, zaidi ya watu 74,500 wameambukizwa virusi vya Covid-19 nchini China. Kwingineko ulimwenguni, nchi 25 zimekubwa na ugonjwa huo, ikiwa ni pamoja na Iran ambayo imetangaza vifo vya wati wawili.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.