Pata taarifa kuu
CHINA-JAPANI-KOREA KUSINI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Hali ya wasiwasi yatanda Japani na Korea Kusini, China yaanza kuwa na matumaini

China imetangaza kesi mpya 394 za maambikizi ya virusi vya Covid-19, ishara kwamba sasa maambukizi hayo yameanza kupunguwa kwa kiwango cha kuridhisha, imesema Wizara ya Afya ya China.
China imetangaza kesi mpya 394 za maambikizi ya virusi vya Covid-19, ishara kwamba sasa maambukizi hayo yameanza kupunguwa kwa kiwango cha kuridhisha, imesema Wizara ya Afya ya China. REUTERS

China imekaribisha hali ya kupunguwa kwa kesi mpya za maambukizi ya virusi vya ugonjwa unaofahamika sasa Covid-19 (Corona), lakini wasiwasi umeongezeka nchini Japan kutokana na vifo vya abiriwa wawili walioambukizwa virusi hivyo kwenye meli iliyozuiliwa kwenye Pwani ya Yokohama.

Matangazo ya kibiashara

Korea Kusini pia imebaini kwamba ina wasiwasi mkubwa, baada ya kesi mpya za maabukizi kuripotiwa.

Tume ya kitaifa (Wizara) ya Afya imeripoti vifo vya watu 114 walioambukizwa virusi vya ugonjwa wa Covid-19 nchini China ndani ya muda wa saa 24, na kusababisha idadi ya vifo kote nchini humo (ukiondoa Hong Kong na Macao) kufikia 2,118.

Lakini imetangaza kesi mpya 394 za maambikizi ya virusi vya Covid-19, ishara kwamba sasa maambukizi hayo yameanza kupunguwa kwa kiwango cha kuridhisha, imesema Wizara ya Afya ya China.

Kwa jumla, zaidi ya watu 74,500 wameambukizwa virusi vya Covid-19 nchini China. Kwingineko ulimwenguni, nchi 25 zimekubwa na ugonjwa huo, ikiwa ni pamoja na Iran ambayo imetangaza vifo vya wati wawili.

Nchini Japani, hali bado ni ngumu baada ya kuripotiwa vifo vya watu wawili walioambikizwa virusi hivyo waliokwama katika meli ya Diamond Princess, iliyowekwa karantini kwenye pwani ya Yokohama, nchini humo.

Katika nchi jirani ya Korea Kusini, ambapo idadi ya watu walioambukizwa virusi vya ugonjwa wa Covid-19 imeongezeka maradufu ndani ya muda wa saa 24 zilizopita, hadi 104. Mtu wa miaka 60, aliyeambukizwa virusi vya ugonjwa huo hatari, alifariki dunia siku ya Jumatano katika Kaunti ya Cheongdo, kilomita 320 Kusini mwa Seoul.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.