Pata taarifa kuu
CHINA-ITALIA-WHO-AFYA

WHO yatoa wito kwa dunia kujiandaa kwa 'uwezekano wa janga la virusi vya Corona'

Maafisa wa afya wakipulizia dawa kwenye eneo ambalo watu waligunduliwa na ugonjwa wa Corona huko Daegu, Korea Kusini Februari 20, 2020.
Maafisa wa afya wakipulizia dawa kwenye eneo ambalo watu waligunduliwa na ugonjwa wa Corona huko Daegu, Korea Kusini Februari 20, 2020. AFP/Yonhap

Katika muda wa siku chache, idadi ya watu walioambukizwa virusi vya ugonjwa hatari wa Covid-19 imeongezeka katika nchi nyingi. Italia, nchi iliyoathirika zaidi barani Ulaya na ya tatu baada ya China na Korea Kusini, idadi ya kesi za maambukizi iliongezeka kutoka sita siku ya Ijumaa Februari 21 hadi 219 siku nne baadaye.

Matangazo ya kibiashara

Na katika nchi hii kumeripotiwa vifo vya watu sita. Shirika la Afya duniani, WHO, linasema lina wasiwasi mkubwa kutokana na kuongezeka kwa kesi za maambukizi katika nchi nyingi duninia na sasa lina hofu kuwa ugonjwa huo unaweza kuwa "janga" kwa dunia.

Shirika la Afya Duniani, WHO, linasema ni mapema sana kuuita mlipuko wa virusi hivyo janga lakini nchi zinapaswa kuwa katika "awamu ya maandalizi".

"Lazima tuangalie hatua za kukabiliana dhidi ya ugonjwa wa Covid-19, huku tukijiandaa kwa uwezekano wa janga la virusi vya Corona," mkurugenzi mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus alisema Jumatatu hii Februari 24 baada ya kesi mpya za maambukizi kuripotiwa katika nchi nyingi kama Italia, Korea Kusini na Iran pamoja na majirani zake wa Ghuba.

"Janga ni pale maambukizi ya ugonjwa yanaposambaa kwa urahisi kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine katika maeneo mengi ya dunia, " amebaini Tedros Adhanom Ghebreyesus.

Mkuu wa shirika la Afya Duniani, WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus aliwaambia waandishi wa habari Jumatatu kwamba idadi ya visa vya Corona katika siku za hivi karibuni katika mataifa ya Iran, Italia na Korea Kusini vina "tisha sana''.

Zaidi ya visa 1,200 vimethibitishwa katika nchi 30 na kumekuwa na vifo zaidi ya 20. Italia iliripoti vifo vinne zaidi Jumatatu, na kuifanya idadi ya vifo nchini humo kufikia watu saba.

Uwiano wa watu walioathirika waliokufa kutokana na Covid-19 vinaonekana kuwa kati ya 1% na 2%, ingawa WHO inaonya kwamba kiwango cha vifo hakijafahamika bado.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.