Pata taarifa kuu
CHINA-CORONA-AFYA

Coronavirus: Idadi ya vifo yazidi 2,700 nchini China Bara

China inaendelea kupambana dhidi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa unaofahamika kama Covid-19 (Corona).
China inaendelea kupambana dhidi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa unaofahamika kama Covid-19 (Corona). PHILIP FONG / AFP

Watu 78,064 wameambukizwa virusi vya ugonjwa hatari unaofahamika sasa kama Covid-19 na kusababisha vifo vya watu 2,715 nchini China Bara tangu ugonjwa huo ulipozuka mwezi Desemba mwaka jana, viongozi wa afya nchini China wamesema katika taarifa yao ya kila siku kuhusu janga hilo.

Matangazo ya kibiashara

Tume ya kitaifa ya Afya imesema imeorodhesha vifo vipya 52 vilivyotokana na maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa Covid-19 nchini China Bara Jumanne wiki hii, ukilinganisha na vifo 71 vya siku moja iliyopita.

Tume hiyo imetangaza kesi mpya 406 za maambukizi ya virusi hivyo nchini China Bara, ikilinganishwa na 508 siku moja iliyopita.

Jumla ya vifo vipya na kesi mpya za maambukizi vimeripotiwa katika mkoa wa Hubei, katikati mwa nchi, ambapo ugonjwa huo ulianza.

Mikoa kadhaa ya China imetangaza Jumatano wiki hii kwamba watarekebisha hatua zao za dharura dhidi ya janga hilo, wakisema kwamba hatari zinazohusiana na virusi hivyo zimepungua.

Kiwango cha tahadhari, ambacho kwa sasa kiko juu zaidi (kiwango cha 1), kitakwenda hadi kiwango cha 2, hasa katika mji wa Sichuan na Xinjiang, vyombo vya habari nchini China vimeripoti.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.