Pata taarifa kuu
UNSC_CORONA-AFYA

Covid-19: Baraza la Usalama la UN lazitaka nchi kutafutia pamoja jawabu kuhusu Corona

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa azitaka nchi kuungana katika vita dhidi ya Corona.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa azitaka nchi kuungana katika vita dhidi ya Corona. Yuri KADOBNOV / AFP

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, amelitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lililogawanywa kwa muda wa wiki kadhaa, kuungana dhidi ya janga la Covid-19, akisisitiza kwamba ni "mapambano yanayohusu nchi zote duniani.

Matangazo ya kibiashara

"Ishara ya umoja na uamuzi kwa upande wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ni katika kipindi hiki cha sasa chenye wasiwasi mkubwa," Antonio Guterres amesema wakati wa mkutano wake wa kwanza kuhusu janaga hil, kupitia video.

Kikao hicho, kilichofanyika katika faragha, kilimalizika baada ya masaa matatu kwa taarifa ya mistari michache kutoka kwa wanachama 15 wa baraza hilo, iliyoonesha "uungwaji wao mkono" kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.

Katika siku zijazo, "hatua za Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa zitakuwa muhimu kupunguza athari kuhusu amani na usalama kwa janga la Covid-19". "Ili kuondokana na janga hili leo, tunahitaji kufanya kazi kwa pamoja" na "hiyo inamaanisha kuimarisha mshikamano," amesisitiza Antonio Guterres, akitoa mfano wa hatari zingine za ugaidi ambazo "bado zipo".

Kwa niaba ya Marekani, Balozi Kelly Craft alirejelea mvutano kati ya China na Marekani kuhusiana na virusi vya Corona, ambavyo vilianzia China, suala tete ambalo limeleta mgawanyiko kwenye barazo hilo .

"Njia bora zaidi ya kudhibiti janga hili ni kukusanya data sahihi kulingana na data ya kisayansi na kutathmini vyanzo vyake, tabia na kuenea kwa virusi hivi," alisema, katika hotuba yake iliyotolewa na wasaidizi wake.

Mwenzake wa Wachina, Zhang Jun, alisema kwa upande wake kwamba "vitendo vyote vya unyanyapaa na siasa vinapaswa kufutiliwa mbali".

Idadi ya visa vya maambukizi ya virusi hivyo kote duniani tangu vilipoanza kusambaa kutokea China mapema mwaka huu imefika milioni 1.5 kwa mujibu wa takwimu za shirika la habari la AFP. Watu zaidi ya 88,981 wamefariki dunia.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.