Pata taarifa kuu
BOLIVIA-Uchaguzi-siasa

Bolivia: Evo Morales rais kwa muhula wa tatu

Evo Morales ambaye amechaguliwa rais kwa muhula wa tatu kuiongoza Bolivia, akiwa mbele ya Ikulu mjini La Paz, Oktoba 12 mwaka 2014.
Evo Morales ambaye amechaguliwa rais kwa muhula wa tatu kuiongoza Bolivia, akiwa mbele ya Ikulu mjini La Paz, Oktoba 12 mwaka 2014. REUTERS/Gaston Brito

Kulingana na matokeo ya kwanza ya muda, rais anaye maliza muda wake, Evo Morales amechaguliwa kwa mara nyingine tena kuingoza Bolivia kwa muhula wa tatu.

Matangazo ya kibiashara

Matokeo hayo yanaonesha kuwa rais Morales amepata asilimia 60 ya kura, akimshinda mpinzani wake Samuel Doria Medina ambaye amepata asilimia 25 ya kura.

Upande wa wabunge, chama cha kiongozi huyo wa kisoshalisti MAS kimepata theluthi mbili ya viti, lakini matokeo hayo yanasubiri tu kuthibitishwa.

Kiongozi wa zamani wa mrengo wa Kulia, Jorge Quironza, amepata asilimia 9. Evo Morales amemshinda kiongozi huyo katika jimbo la santa Cruz, ambalo linakaliwa na wafuasi wengi wa upinzani kutoka mrengo wa Kulia.

Watu takribani milioni 6 wameshiriki uchaguzi huo, ambao nchini bolivia ni amri. Uchaguzi huo umefanyika katika hali ya utulivu

Baada ya kutangaza mataokeo ya mwanzo, Evo morales amesema ushindi wake ni kwa niaba ya rais wa zamani wa Cuba Fidel Castro pamoja na hayati rais wa Venezuela hugo Chavez.

Katika uongozi wake, Morales amekuwa akisifiwa kwa kuimarisha uchumi wa nchi yake, kuimarisha usalama na kupunguza umasikini nchini mwake mambo ambayo yamempa umaarufu mkubwa.

Wafuasi wa Evo Morales wakisheherekea ushindi mjini La Paz Oktoba 12 mwaka 2014.
Wafuasi wa Evo Morales wakisheherekea ushindi mjini La Paz Oktoba 12 mwaka 2014. REUTERS/Gaston Brito

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.