Pata taarifa kuu
BRAZIL-USALAMA

Bwawa laporomoka, watu 17 wapoteza maisha

Manusura wa maporomoko ya matope, Novemba 5, 2015 katika kijiji cha Bento Rodrigues nchini Brazil.
Manusura wa maporomoko ya matope, Novemba 5, 2015 katika kijiji cha Bento Rodrigues nchini Brazil. AFP/AFP

Kwa uchache watu 17 wamepoteza maisha na zaidi ya 50 wamejeruhiwa Alhamisi hii nchini Brazil baada ya kuporomoka kwa bwawa la madini ambalo limesababisha kuporomoka kwa matope makubwa na kuvamia kijiji kimoja, maafisa wa zima moto wameliambia shirika lahabari la Ufaransa la AFP.

Matangazo ya kibiashara

" Watu 17 wamepoteza maisha. Idadi ya watu waliokosekana itazidi 40, lakini idadi hii bado haijawa rasmi ", Adao Severino Junior, Mkuu wa wazima moto wa mji wa Mariana (kusini) amesema.

" Idadi ya majeruhi imezidi 50", afisa huyo mwandamizi ameongeza, akizungumza kwa njia ya simu kutoka katika moja ya vijiji viliyovamiwa na matope.

Mwili wa afisa wa Zima Moto wa eneo la Ouro Preto, mji mwingine wa karibuuliyokumbwa na hali hiyo, pia imepelekea idadi ya watu waliopoteza maisha kufikia 17, kwa mujibu wa radio na mtandao wa Bandnews.

Katika ripoti ya awali iliyotolewa na kiongozi wa wachimbaji migodi ilisema kuwa mtu mmoja ndiye aliuawa na wengine watano walijeruhiwa.

" Hii ni hali tete. Kuna giza. Kuna matope mengi. zoezi la kutafuta miili ya watu waliopoteza maisha litaendelea usiku kucha ", Mkuu wa wazima moto wa eneo la Mariana ameongeza.

Watu waliojeruhiwa wamepelekwa hospitali katika eneo la Mariana na mji wa Santa Rita Durao, Adao Severino Junior amesema.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.