Pata taarifa kuu
BRAZILI-SIASA-UCHUMI

Brazil: Wabunge wapiga kura ya kumtimua Dilma Rousseff

Wabunge wanaomuunga mkono Dilma Rousseff wakionyesha msimamo wao.
Wabunge wanaomuunga mkono Dilma Rousseff wakionyesha msimamo wao. REUTERS/Ueslei Marcelino

Chama cha mrengo wa kushoto cha Dilma Rousseff kimekubali kushindwa Bungeni Jumapili hii usiku. Wabunge wa Brazil wamepiga kura ya kumng'oa mamlakani rais kutoka chama cha mrengo wa kushoto katika kikao cha kihistoria. Kwa hiyo utaratibu utaendelea katika Baraza la Seneti.

Matangazo ya kibiashara

Dilma Rousseff amepoteza vita muhimu katika mapambano yake kwa kuendelea kuwa rais wa Brazil. Wabunge wamepiga kura ya muendelezo wa utaratibu wa kumtimua mamlakani rais Rousseff.

Hoja ya upinzani ilionekana kuungwa mkono mapema jioni, wakati ambapo Wabunge walikua wengi wakipanga mistari mbele ya kipaza sauti kwa kupiga kura zao, mwandishi wetu katika mji wa Brasilia, Martin Bernard, amearifu.

Kiongozi wa Chama cha Wafanyakazi cha Dilma Rousseff katika Baraza la Wawakilishi amekubali kushindwa kwa kambi ya rais kabla hata ya kumalizika kwa zoezi la kupiga kura.

Vita vinaendelea katika Baraza la Seneti

Idadi iliyokua inahitajika ya kumtimua imezidi theluthi mbili ya kura (342 ya 513), na sasa utaratibu huu unaendelea katika Baraza la Seneti.

Baraza la Seneti litaidhinisha au la kumng'atuliwa madarakani kwa rais kutoka chama cha mrengo wa kushoto. Rais Dilma Russeff, madarakani tangu mwaka 2010, anatuhumiwa na upinzani kutumia pesa za umma katika uchaguzi wake mwaka 2014. Utaratibu utajadiliwa katika Baraza la Seneti kuanzia Jumatatu. BAraza la Seneti ndi litakua na uamuzi wa mwisho.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.