Pata taarifa kuu
VENEZUELA-MAANDAMANO-USALAMA

Vijana waendelea na maandamano nchini Venezuela

Wafuasi wa upinzani nchini Venezuela wakati wa makabiliano na vikosi vya usalama Aprili 26, 2017 mjini Caracas.
Wafuasi wa upinzani nchini Venezuela wakati wa makabiliano na vikosi vya usalama Aprili 26, 2017 mjini Caracas. REUTERS/Marco Bello

Nchini Venezuela, uhamasishaji dhidi ya Rais Maduro unaendelea. Siku ya Jumatano Aprili 26 na vijana, katika miji mbalimbali, walishiriki maandamano ya kudai rais Maduro ajiuzulu.

Matangazo ya kibiashara

Idadi ya watu waliopoteza maisha katika maandamano hayo yanayoendelea nchini humo imeongezeka. Kijana mmoja alipoteza maisha katika mji wa Caracas baada ya kurushiwabomu ya kutoa machozi katika maandamano yaliyoitishwa na upinzani.

Jumla ya watu 29 walipoteza maisha katika machafuko hayo yalitoanza tangu mwanzoni mwa mwezi Aprili nchini Venezuela, ikiwa ni pamoja na watu 18 waliouawa wakati wa maandamano ya wafuasi wa upinzani na wale wanaoiunga mkono serikali. Watu wengine 11 walipoteza maisha katika visa vya uporaji katika maduka usiku wa Alhamisi iliyopita katika eneo la kusini magharibi mwa mji wa Caracas.

Maelfu ya wafuasi wa upinzani, hasa vijana, waliangamana siku ya Jumatano na walijaribu kufika katikati ya mji mkuu ili kudai kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu nchini humo. Kwa upande mwingine, rais Nicolas Maduro aliwatolea wito wafuasi wake, hasa vijana, kuingia mitaani siku ya Jumatano katika mji wa Caracas "kwa maandamano ya amani."

Tangu Mahakama Kuu ilipotoa uamuzi wa kutambua mamlaka ya Bunge ambapo upinzani una idadi kubwa ya wabunge, vijana na wanafunzi wa Vyuo Vikuu walionekana kwa wingi katika maandamano hayo yanayoendelea.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.