Pata taarifa kuu
VENEZUELA-MAANDAMANO-USALAMA

Rais Venezuela anyooshewa kidole cha lawama

Wafuasi wa upinzani wakati wa makabiliano na vikosi vya usalama Aprili 26, 2017 katika mji wa Caracas, Venezuela.
Wafuasi wa upinzani wakati wa makabiliano na vikosi vya usalama Aprili 26, 2017 katika mji wa Caracas, Venezuela. REUTERS/Marco Bello

Marekani na Umoja wa Ulaya zimeshtumu rais wa Venezuela Nicolas Maduro kwa kuwaminya wapinzani.

Matangazo ya kibiashara

Rais Donald Trump amesema Venezuela imepoteza mwelekeo kutokana na maandamano yanayoendela kushinikiza kujiuzulu kwa rais Maduro.

Maandamano nchini Venezuela yamesababisha vifo vya watu 28, huku serikali ikiyashtumu Mataifa ya Magharibi kwa kuchochea maandamano hayo.

Hata hivyo upinzani umeapa kuendelea na maandamano hadi rais wa Venezuela, Nicolas Maduro atapojiuzulu.

Hivi karibuni, Rais Maduro aliomba mazungumzo na upinzani ili kukomesha maandamano hayo.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.