Pata taarifa kuu
BRAZIL-LULA-HAKI

Lula ahukumiwa kifungo cha zaidi ya miaka 9 jela kwa kashfa ya rushwa

Aliekua rais wa Brazil anashtumiwa kuhusika katika kashfa ya rushwa ya Petrobras ambayo imeendelea kutikisa nchi hiyo kwa miaka kadhaa.
Aliekua rais wa Brazil anashtumiwa kuhusika katika kashfa ya rushwa ya Petrobras ambayo imeendelea kutikisa nchi hiyo kwa miaka kadhaa. REUTERS/Paulo Whitaker

Aliekua rais wa Brazil Lula da Silva alihukumiwa siku ya Jumatano Julai 12 zaidi ya miaka 9 jela kwa kosa la rushwa. Kiongozi huyo muhimu wa mrengo wa kushoto, Luiz Inacio Lula da Silva, ambaye alikuwa akiongoza Brazil tangu mwaka 2003 hadi 2010, atasalia nje ya gereza mpaka kesi yake itakapofikishwa katika mahakama ya rufaa.

Matangazo ya kibiashara

Rais huyo wa zamani wa Brazil alipatikana na hatia ya kupokea rushwa ya Euro zaidi ya milioni moja, alihukumiwa kwa kosa la rushwa na kujitajirisha kinyume cha sheria

Bw Lula da Silva alikutwa na hatia ya kukubali hongo ya zaidi ya dola milioni moja za malipo ya ghorofa ya mapumziko kwa ajili ya ukarabati wake kwa kampuni ya ujenzi ya Brazil, OAS, ikiwa ni kashfa kubwa ya rushwa katika historia ya nchi hiyo.

Kwa mujibu wa jaji Sergio Moro, mashahidi wawili wamethibitisha kuwa Lula aliomba kwamba ushahidi wa manunuzi upotezwe.

Kiongozi huyo wa zamani wa chama cha muungano alijizolea umaarufu kutoka jamii ya kimataifa kwa sera zake za kijamii ambazo zilisaidia kuboresha maisha Brazil.

Hukumu hii inakuja wakati ambapo mtawala Lula akiwa ametoa msimamo mkali kwamba ana mpango wa kuingia katika kinyang'anyiro cha kugombea nafasi ya urais mwakani .

Kufuatia hukumu hiyo, rais huyo amekana mashtaka yote yanayomkabili kwa kudai kuwa hajafanya makosa yoyote kiasi cha kustahili hukumu hiyo.

Hata hivyo mawakili wake wamesema watakkata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.