Pata taarifa kuu
VENZUELA-HAKI

Mwendesha mashitaka wa zamani Luisa Ortega amshambulia maduro

Mwanasheria mkuu wa zamani wa Venezuelan Luisa Ortega katika mkutano wa Mercosur Brasilia tarehe 23 Agosti 2017.
Mwanasheria mkuu wa zamani wa Venezuelan Luisa Ortega katika mkutano wa Mercosur Brasilia tarehe 23 Agosti 2017. REUTERS/Ueslei Marcelino

Aliye kuwa mwendesha mashitaka mkuu nchini Venezuela amemshtumu rais wa nchi hiyo kujihusisha na rushwa kwa ushirikiano na maafisa wengi wakuu.

Matangazo ya kibiashara

Katika mkutano wa mawakili wakuu wa Mercosur mjini Brasilia siku ya Jumatano, Agosti 23, Luisa Ortega, ambaye alikimbilia Colombia na kisha Brazil baada ya kufutwa kazi na bunge jipya la Katiba la Venezuela, alisema ana ushahidi wa rushwa dhidi ya rais Nicolas Maduro na maafisa wengine wakuu. Amesema aliteswa na anahofia maisha yake, huku akilaani kuwa "sheria inavunjwa kwa maksudi" katika nchi yake.

Haya ni mashtaka makubwa dhidi ya serikali ya venezuela. Luisa Ortega ameshutumu mfumo wa rushwa unaotumiwa kwenye ngazi za juu serikalini.

Kwa mujibu wa Bi Ortega, ambaye kwa sasa ni hasimu mkuu wa rais Nicolas Maduro, mamlaka nchini Venezuela inamtafuta "kwa lengo la kuficha mengi kuhusu rushwa ambapo ana mengi kuhusu ushahidi."

"Na kwa kweli, ameongeza mwendesha mashitaka mkuu wa Venezuela ambaye alikimbia Colombia baada ya kutimuliwa kwenye nafasi yake katika kesi ya kashfa ya Odebrecht. Nina ushahidi unaowahusisha viongozi wengi waandamizi nchini Venezuela, pamoja na rais na wajumbe wa Bunge jipya la Katiba, Diosdado Cabello na Jorge Rodriguez. "

Kwa mujibu wa Luisa Ortega, Diosdado Cabello, mshirika wa karibu wa rais Nicolas Maduro alipokea dola milioni 100 kutoka kampuni ya Brazil ya Odebrecht.

Mwendesha mashitaka mkuu wa zamani anaomba jumuiya ya kimataifa kuchunguza kuhusu rushwa nchini Venezuela. Ameahidii kutoa taarifa alio nazo kwa viongozi wa nchi kadhaa, ikiwa ni pamoja na Marekani.

Mwendesha mashitaka mkuu mpya Tarek Saab ambaye anatuhumiwa pia na Ortega anasema kuwa madai hayo hayana msingi.

Tarek Saab amemkosoa Bi Ortega kwamba alifukuzwa utumishi serikalini kutokana na kufanya vitendo kinyume na maadili na kwamba ndani ya miaka kumi akiwa kazini ameshindwa kuchunguza tuhuma za rushwa.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.