Pata taarifa kuu
MEXICO-USALAMA

Watu 13 wapoteza maisha katika makabiliano gerezani nchini Mexico

Moshi ukifumba katika gereza la Cadereyta wakati ambapo makabiliano kati ya makundi mawili hasimu ya wafungwa yakishuhudiwa ndani ya gereza hilo, Oktoba 10, 2017, Mexico.
Moshi ukifumba katika gereza la Cadereyta wakati ambapo makabiliano kati ya makundi mawili hasimu ya wafungwa yakishuhudiwa ndani ya gereza hilo, Oktoba 10, 2017, Mexico. Julio Cesar AGUILAR/ AFP

Wafungwa wasiopungua 13 walipoteza maisha gerezani siku ya Jumanne kaskazini mwa Mexico, kufuatia mapigano yaliyozuka kati ya wafungwa, chanzo cha serikali kimesema.

Matangazo ya kibiashara

Tukio hilo lililotokea katika gereza la Cadereyta, kaskazini mwa Nuevo Leon, ambapo makabiliano kati ya makundi hasimu ya wafungwa yalisababisha vifo vya watu 49 mwaka jana katika gereza jingine.

Vurugu za siku ya Jumanne ziliua watu 13, wote wafungwa, na uchunguzi unaendelea, amesema msemaji wa idara ya usalama katika jimbo la Nuevo Leon katika mkutano na waandishi wa habari.

tukio hilo lilianza siku ya mapema Jumanne aalfajiri kabla ya hali ya mambo kudhibitiwa, lakini hali hiyo ilirudi kushuhudiwa asubuhi wakati kundi la watungwa 20 walisababisha kilipuka kwa moto katika jela hilo.

Wafungwa wawili waliuawa kwa visu na askari magereza wawili walijeruhiwa, chanzo cha polisi kimesema.

Polisi waliingilia kati katika gereza hilo, liliyo nje ya jiji la Monterrey, jiji la tatu kwa kubwa zaidi la nchi hiyo.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.