Pata taarifa kuu
VENEZUELA-SIASA

Uchaguzi wa rais kufanyika Mei 20 Venezuela

Rais wa Venezuela Nicolas Maduro, katika mkutano na waandishi wa habari, Februari 15 huko Caracas.
Rais wa Venezuela Nicolas Maduro, katika mkutano na waandishi wa habari, Februari 15 huko Caracas. REUTERS/Marco Bello

Uchaguzi wa urais nchini Venezuela ambao awali ulipangwa kufanyika Aprili 22, hatimaye umeahirishwa hadi tarehe 20 Mei 2018, Tume ya Uchaguzi nchini humo (CNE) imetangaza.

Matangazo ya kibiashara

Rais anayemaliza muda wake Nicolas Maduro atawania katika uchaguzi huo kwa muhula wa pili wa miaka sita, kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi, CNE.

Tarehe hii mpya ni matokeo ya makubaliano na mpinzani wa Nicolas Maduro yaliyolenga kuhakikishia jumuiya ya kimataifa, kwa mujibu wa afisa mmoja ambaye hakutaja jina lake.

"Nina furaha kubwa kuona mikataba ilisainiwa na upinzani kwa sababu nataka kwenda kwa mchakato wa maridhiano (...) Twende katika uchaguzi, mimi nina uhakika kwamba tutashinda," amesema Nicolas Maduro katika ujumbe alioandika kwenye ukurasa wake Facebook.

Mikataba hiyo ilitabiriwa kwa siku kadhaa, baada ya Henri Falcon kufichua kuwa kumekuepo na mazungumzo ya siri na serikali. Makubaliano yanajumuisha mambo kadhaa yanayohakikisha uchaguzi wa wazi na wenye kuaminika.

"Tunapendekeza kuwa uchaguzi wa urais ufanyike wa wakati mmoja" na uchaguzi wa halmashauri za mabunge ya kikanda, kulingana na makubaliano yaliyofikiwa, na kuidhinishwa na Tume ya Uchaguzi (CNE).

Uchaguzi wa rais, ambao kawaida ungelifanyika mwezi Desemba mwaka jana uliahirishwa hadi mwezi Aprili na Tume ya Uchaguzi. Uamuzi uliokosolewa na baadhi ya nchi za jumuiya ya kimataifa na muungano mkuu wa upinzani ambao uliamua kususia uchaguzi huo.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.