Pata taarifa kuu
VENEZUELA

Wafungwa 68 wapoteza maisha Venezuela wakijaribu kutoroka

Moja ya wazazi na mwanae wakilia nje ya jela ambayo imeungua moto usiku wa kuamkia leo nchini Venezuela. 28.03.2018 28 mars 2018.
Moja ya wazazi na mwanae wakilia nje ya jela ambayo imeungua moto usiku wa kuamkia leo nchini Venezuela. 28.03.2018 28 mars 2018. REUTERS/Carlos Garcia Rawlins

Watu 68 wamekufa nchini Venezuela wakati walipojaribu kutoroka kwenye jela moja baada ya moto kuzuka kwenye vyumba ambavyo walikuwa wakizuiliwa na Polisi, hili likiwa tukio baya zaidi kuripotiwa kwenye jela lenye ulinzi mkali na lenye idadi kubwa ya wafungwa.

Matangazo ya kibiashara

Mwanasheria mkuu wa Serikali Tarel William ametoa idadi hii usiku wa kuamkia leo kwenye makao makuu ya polisi kaskazini mwa mji wa Carabobo, akilaumu kuwa moto huo uliwashwa kwa makusudi.

Carlos Nieto mkuu wa gereza hilo amesema baadhi ya wafungwa waliungua hadi kufa na wengine kwa kukosa hewa baada ya moto kuanza kuunguza magodoro na kuanza kuiba slaha kutoka kwa walinzi wakijaribu kutoroka.

Miongoni mwa waliokufa ni wanawake wawili ambao walienda kuwatembelea ndugu zao, amesema mwanasheria mkuu ambaye amedai kuwa waendesha mashtaka wanne wameteuliwa kuchunguza tukio hili.

Picha zilizopigwa na vuguvugu la Nieto limeonesha askari wa zima moto wakijaribu kumuokoa mfungwa mmoja aliyekuwa akiungua.

Ndugu wa watu waliokuwa wanazuiliwa kwenye kituo kimoja walilazimisha kuingia baada ya polisi mmoja kupigwa jiwe ambapo baadae polisi walilazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya.

Video iliyotumwa kwenye mtandao wa kijamii wa twitter umeonesha mamia ya watu wakiomba kupewa taarifa kutoka kwa polisi waliokuwa wanalinda jela hiyo huku wanawake wakilia.

"Nina hofu. Mwanangu amekuwa hapa kwa karibu wiki moja. Hawajanipa taarifa zozote,: alisema Dora Blanco.

Wafungwa wengi nchini Venezuela wanataabika kutokana na hali mbaya za magereza, kukosekana kwa mahitaji muhimu ya kibinadamu na jela kujaa kupita kiwango huku wakikabiliwa na hali mbaya ya kiuchumi.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.