Pata taarifa kuu
MAREKANI-TRUMP-SIASA

Mwanasheria binafsi wa Trump kuripoti Mahakamani Jumatatu

Michael Cohen, mwanasheria binafsi wa Donald Trump.
Michael Cohen, mwanasheria binafsi wa Donald Trump. /fr.news.yahoo.com

Michael Cohen, mwanasheria binafsi wa Donald Trump, na mshirika wake wa muda mrefu, anatazamiwa kufikishwa mahakamani mjini New York leo Jumatatu. Cohen alikiri kumlipa nyota wa filamu za ngono Dola130,000 ( sawa na £95000) mwaka 2016, akibaini kwamba alikua na uhusiano wa kimapenzi na rais wa Marekani.

Matangazo ya kibiashara

Katika hati iliyotolewa siku ya Ijumaa katika mahakama ya Manhattan, waendesha mashitaka wanasema Cohen anakabiliwa na uchunguzi wa makosa ya jinai kwa miezi kadhaa. Uchunguzi huu unahusu "shughuli za biashara binafsi" za Michael Cohen zaidi ya taaluma yake ya kisheria.

Mapema wiki iliyopita maofisa wa Shirika la Upelelezi la FBI walifanya uvamizi kwenye ofisi ya mwanasheria binafsi wa Rais donald Trump huko New York, nyumbani kwake na chumba cha hoteli, na kuchukua mfululizo wa nyaraka.

Wanasheria wa Cohen wamebaini kwamba stakabadhi zilizochukuliwa na wachunguzi wa FBI haziwezi kuwekwa kwenye uchunguzi kutokana na siri ya kitaaluma inayohusu uhusiano kati ya wakili na wateja wake.

Katika kikao cha siku ya Ijumaa, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Tom McKay alisema wanasheria wa Cohen walielezea kimakosa kipengele hicho.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.