Pata taarifa kuu
GUATEMALA-VOLKANO-USALAMA

Zaidi ya 25 wapoteza maisha kufuatia mlipuko wa volkano Guatemala

Polisi wakimuokoa mtu aliyejeruhiwa wakati wa mlipuko wa volkano ya Fuego, katika kijiji cha El Rodeo, kilomita 35 kusini mwa mji mkuu wa Guatemala, tarehe 3 Juni 2018.
Polisi wakimuokoa mtu aliyejeruhiwa wakati wa mlipuko wa volkano ya Fuego, katika kijiji cha El Rodeo, kilomita 35 kusini mwa mji mkuu wa Guatemala, tarehe 3 Juni 2018. AFP

Watu zaidi ya 25 wamepoteza maisha na 20 wamejeruhiwa nchini Guatemala kufuatia mlipuko wa volkano nchini Guatemala, idara inayokabiliana na majanga nchini humo imesema.

Matangazo ya kibiashara

Awali serikali ya Guatemala imesema kuwa majivu ya volkano kutoka mlima mmoja unaoendelea kulipuka, yamesababisha vifo vya watu saba na kuwajeruhi wengine ishirini.

Mlipuko wa Volkano ya Fuego (Volkano ya moto), inayopatikana kilomita 35 kusini-magharibi mwa mji mkuu wa Guatemala, umesababisha maelfu ya watu na kuhamishwa na uwanja wa ndege wa kimataifa umetakiwa kufungwa.

Serikali ya Guatemala inasema kuwa takribani watu milioni moja wameathirika kutokana na Volcano hiyo.

Hata hivyo ushauri umetolewa kwa raia kuvaa vifaa vya kuzuia pua zao kutokana na moshi na majivu yanayoendelea kurushwa kutokana na Volcano hiyo.

Mlipuko huo umeathiri hasa wilaya za vijijini zilizo karibu na volkano hiyo na mji wa kikoloni wa Antigua, eneo muhimu kwa utalii nchini Guatemala.

Kulingana na ripoti mpya, watu zaidi ya 25 ndio wamepoteza maisha, watoto kadhaa ni miongoni mwa watu waliopoteza maisha, amesema msemaji wa idara ya ya kitaifa inayokabiliana na majanga (Conred), David de Leon.

Amesema kuwa watu 25 walioppteza maisha walipatikana katika maeneo mawili yalio karibu na volkano, El Rodeo na Las Lajas.

Rais wa taifa hilo Jimmy Morales amesema vikosi vya uokoaji vimeanza kazi na tahadhari imetolewa.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.